Home Dauda TV DAUDA TV: ANGALIA JKT RUVU ILIVYOTOA KISAGO KWA TANZANIA PRISONS

DAUDA TV: ANGALIA JKT RUVU ILIVYOTOA KISAGO KWA TANZANIA PRISONS

582
0
SHARE

IMG-20151213-WA0038

Jana ilipigwa michezo miwili ya ligi kuu ya Vodacom Tazanzania bara mchezo wa kwanza ulikuwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kati ya JKT Ruvu dhidi ya Tanzania Prisons na mwingine ulikuwa jijini Tanga (Tanga Derby) kati ya African Sports dhidi ya Coastal Union mchezo huo ukisukumwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Camera ya Dauda TV ilikuwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiangazia mchezo kati ya JKT Ruvu dhidi ya Tanzania Prisons na kushuhudia mchezo huo ukimalizika kwa JKT Ruvu kupata ushisi wa magoli 4-1 dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza kutoka jijini Mbeya.

Michael Aidani alikuwa shujaa wa JKT Ruvu baada ya kupiga magoli matatu (hat-trick) na kuisaidia timu yake kuibuka na paointi tatu muhimu.

Bao pekee la Tanzania Prisons lilifungwa na Mohamed Mpoki kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo kumalizika kwa JKT Ruvu kuibuka na ushindi wa goli 4-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here