Home Kimataifa SAMATTA, ULIMWENGU WATUPWA NJE KOMBE LA DUNIA

SAMATTA, ULIMWENGU WATUPWA NJE KOMBE LA DUNIA

608
0
SHARE
Samatta-JPN
Kikosi cha TP Mazembe ambacho kinaundwa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kimeenguliwa kwenye michuano ya FIFA Club World Cup inayoendelea kuchanja mbuga nchini Japan baada kukubali kipigo cha magoli 3-0 mbele ya wenyeji Sanfrecce Hiroshima kwenye mchezo uliomalizika kwenye dimba la Osaka Nagai Stadium, Japan.
Wachezaji wa Sanfrecce Hiroshima pamoja na wa TP Mazembe wakiingia uwanjani tarari kwa mechi
Wachezaji wa Sanfrecce Hiroshima pamoja na wa TP Mazembe wakiingia uwanjani tarari kwa mechi

Timu zote zilianza mchezo kwa kasi tangu kupulizwa filimbi ya kwanza. Lakini Sanfrecce walianza kufumania nyavu za mazembe dakika ya 44 kipindi cha kwanza kupitia kwa Shiotani baada ya Yusuke Chajima kupiga mpira wa kona uliotua kichwani kwa Sho Sasaki kisha kumkuta Shiotani aliyefunga kwa shuti la karibu.

Thomas Ulimwegu wa TP Mazembe akiachia shuti
Thomas Ulimwegu wa TP Mazembe akiachia shuti

Kikosi cha Mazembe kilizinduka na kuanza kutafuta goli la kusawazisha ambapo Assale alionekana kuwa mwiba kwa upande wa Sanfrecce ambapo alimjaribu golikipa wa Takuyo Hayashi mara mbili kwa mashauti ya mbali bila mafanikio.

Richard Boateng waTP Mazembe na Douglas wa Sanfrecce Hiroshima wakiwania mpira
Richard Boateng waTP Mazembe na Douglas wa Sanfrecce Hiroshima wakiwania mpira

Thomas Ulimwengu aliingia kipindi cha pili na ilibaki kidogo afunge goli muda mfupi baada ya kuingia  baada ya kukimbia na mpira kwa kasi takribani mita 40 na kuachia shuti kali ambalo lilitoka centimeter chache nje ya goli. Alipiga pia mpira wa adhabu ndogo ambao haukuzaa matunda wakati mabingwa hao wa bara la Afrika wakiwa kwenye harakati za kusaka goli la kusawazisha

Dakika ya 56 Kazuhiko Chiba alifunga bao la pili akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Chajima na kuzidi kuwaweka Mazembe kwenye wakati mgumu.

Salif Coulibaly wa TP Mazembe akimkabili Douglas wa Sanfrecce Hiroshima
Salif Coulibaly wa TP Mazembe akimkabili Douglas wa Sanfrecce Hiroshima

Asano alizima kabisa ndoto za waafrika za kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kufunga bao la tatu na kuwaacha vijana na tajiri Moise Katumbi wakiwa vichwa chini wasiamini kilichowakuta.

Matokeo hayo yameipa Sanfrecce Hiroshima tiketi ya kufuzu kucheza nusu fainali ya mashindano ya FIFA Club World Cup ambapo watakutana na River Plate kwenye mchezo huo wa nusu fainali.

Kazuhiko Chiba wa Sanfrecce Hiroshima akishangilia baada ya kufunga goli
Kazuhiko Chiba wa Sanfrecce Hiroshima akishangilia baada ya kufunga goli

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here