Home Kimataifa PAULINHO, ROBINHO, SCOLARI, WATAMBA CLUB WORLD CUP JAPAN

PAULINHO, ROBINHO, SCOLARI, WATAMBA CLUB WORLD CUP JAPAN

544
0
SHARE

Japan 3

Na Shaffih Dauda, Osaka, Japan

Guangzhou Evergrande imekata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya FIFA Club World Cup 2015 inayoendelea nchini Japan baada ya Paulinho kufunga kwa kichwa dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza na kuipa timu yake ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Club America.

Kikosi cha Luiz Felipe Scolari kilianza kwa kusuasua lakini mabadiliko yaliyofanywa na kocha huyo kwa kuwaingiza Zheng Long, Lin Gao na Yu Hanchao yalibadili mchezo huo huku wachezaji wote hao wakihusika katika upatikanaji wa magoli.

Japan 4

Club America ndiyo walianza kupata goli la kwanza lililofungwa na Peralta aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Benedetto.

Dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika, viajana wa Scolari wakasawazisha goli hilo lililofungwa na Long Zheng baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Lin Gao pamoja na Paulinho.

Japan 5

Baada ya kupata goli hilo, mabingwa hao wa Asia walianza kutafuta goli la ushindi na hatimaye juhudi zao zilizaa matunda dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza (90+3). Kona iliyochongwa na Yu Hangchai ilitua kichwani kwa Paulinho aliyekuwa karuka juu na kuzama moja kwa moja wavuni na kupeleka shangwe kwa mashabiki wa China.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here