Home Kimataifa HIKI NDICHO KILICHOSABABISHA TP MAZEMBE KUTUPWA NJE YA MICHUANO YA CLUB WORLD...

HIKI NDICHO KILICHOSABABISHA TP MAZEMBE KUTUPWA NJE YA MICHUANO YA CLUB WORLD CUP, KOCHA AWEKA WAZI KILAKITU

564
0
SHARE
Kocha wa TP Mazembe Patrice Carteron
Kocha wa TP Mazembe Patrice Carteron
Kocha wa TP Mazembe Patrice Carteron
 Na Shaffih Dauda, Osaka, Japan
Baada ya mchezo wa FIFA Club World Cup kumalizika hapa kwenye uwanja wa Osaka Nagai kati ya Sanfrecce Hiroshima dhidi ya TP Mazembe huku ukishuhudiwa mabingwa wa Afrika wakiaga mashandano kwenye hatua ya robo fainali kwa kibano cha goli 3-0 kutoka kwa timu mwenyeji.

Shaffihdauda.co.tz pamoja na timu nzima iliyokita kambi hapa kwenye jiji la Osaka, iliwatafuta makocha wote wa timu mbili na kufanya nao mahojiano kuelezea namna ambavyo mchezo huo ulivyokua pamoja na matokeo ya mchezo huo

Kocha wa TP Mazembe Patrice Carteron amesema kilichopelekea timu yake ipoteze mchezo wa robo fainali ni kukosa umakini kwenye mchezo pamoja na kushindwa kucheza katika ubora wao wa kila siku kama ilivyozoeleka.

“Tumepoteza mchezo muhimu kwetu. Ubora wetu na umakini haukuwepo pamoja na nguvu. Tuliyafanyia kazi hayo kwenye mazoezi na mara nyingi nimekuwa nikizungumza kuhusu umakini kwenye mchezo, lakini mwisho wa siku nimevunjika sana moyo hatukuonesha ubora wetu wa kila siku”, amesema Carteron alipozungumza na Shaffih Dauda muda mfupi baada ya mchezo huo kumalizika.

“Tulifahamu kwamba tunakutana na timu ngumu ambayo mara zote ilionekana hivyo lakini sisi hatukucheza vizuri. Tumepata kile ambacho tunastahili, sina wa kumlaumu. Siku zote ni rahisi kutafuta sababu lakini mimi sina sababu. Ninawapongeza Sanfrecce Hiroshima”.

Kwa upande wa kocha wa Sanfrecce Hiroshima Hajime Moriyasu yeye amewasifia wacheaji wake akisema wamecheza kwa nidhamu ya hali ya juu pamoja na kutekeleza majumu yao kwa usahihi na hiyo ndiyo ilikuwa siri ya ushindi wao.

Kocha wa Sanfrecce Hiroshima Hajime Moriyasu
Kocha wa Sanfrecce Hiroshima Hajime Moriyasu

“Tulifunga goli la kwanza kwa wakati muafaka. Kipindi cha kwanza walikuwa wanatubana sana na kutulazimisha tucheze kwenye nusu yetu ya uwanja na hiyo ikapelekea wapate kona nyingi sana na ikatulaziku kujilinda kwa tahadhari. Japokuwa tulimiliki mpira lakini ilikuwa ni vigumu kwetu kutengeneza nafasi kwasababu ya ubora wao”, amesema Moriyasu.

“Nimefurahishwa na jinsi wachezaji wangu walivyocheza kwa nidhamu ya hali ya juu. Wachezaji wangu walicheza kwa plan yetu walikuwa vizuri na wajanja, kwa asilimia zote tulistahili ushindi”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here