Home Kimataifa EXCLUSIVE INTERVIEW: HIKI NDICHO WALICHOKISEMA SAMATTA NA ULIMWENGU KUELEKEA MECHI YAO YA...

EXCLUSIVE INTERVIEW: HIKI NDICHO WALICHOKISEMA SAMATTA NA ULIMWENGU KUELEKEA MECHI YAO YA KWANZA CLUB WORLD CUP JAPAN

610
0
SHARE

cover

Amini-usiasiami leo watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweka rekodi nyingine tena safari hii siyo Tanzania na Afrika tu, bali safari hii itakuwa ni duniani. Wachezaji hao leo watakuwa ni sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha TP Mazembe kitakachocheza mchezo wa robofainali wa FIFA Club World Cup dhidi ya club ya Sanfrecce Hiroshima ya Japan.

Pambano hilo ambalo endapo TP Mazembe ikishinda inafuzu moja kwa moja kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi duniani kwa ngazi ya vilabu. Pambano hilo litapigwa kwenye dimba la Osaka Nagai Stadium, Japan.

Sanfrecce Hiroshima iliifunga Auckland City 2-0 kwenye mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo na sasa inakutana na mabingwa hao wa Afrika ambao ndiyo timu pekee kutoka Afrika inayoshikilia rekodi ya kufika hatua ya fainali ya mashindano hayo walipocheza dhidi ya Inter Milan na kupoteza kwa goli 3-0 mwaka 2010.

Kama kawaida ya shaffihdauda.co.tz, imefanya mahojiano maalumu na wa-TZ hao Mbwana Samatta pamoja na Thomas Ulimwengu kujua matarajio yao kuelekea mchezo huo. Bila mizengwe nao wakafunguka na kuweka wazi mambo kibao ambayo pengine wewe usingeyajua kirahisi, lakini kwasababu timu ya ushindi ipo kwa ajili yako inakuletea yote hayo karibu yako.

Shaffihdauda.co.tz: Mbwana Samatta ukiwa miongoni mwa watanzania wanaoweka rekodi nyingine ya kuwa watanzania wa kwanza kucheza mechi ya klabu bingwa kwa ngazi ya dunia baada ya kuwa watanzania wa kwanza kucheza fainali ya klabu bingwa Afrika, unaichuikuliaje mechi hiyo kwenye maisha yako ya soka?

Samatta: Binafsi najisikia furaha kuwa kwenye haya mashindano, ni kitu ambacho nilikuwa nakifikiria siku nyingi kama si kukiota, kuwa kwenye mashindano ya namna hii ambayo karibu nusu ya dunia itakuwa inayaangalia mashindano haya. Mimi kama mchezaji kuwa uwanjani nikiangaliwa na karibu nusu ya dunia ni jambo la kujivunia na jambo la furaha sana.

Pili katika maandalizi nimejiandaa vizuri kwa ajili ya hii mechi na kiwango changu sasahivi jinsi kilivyo kiko stable najiamini na nadhani ni mechi ambayo nitafuhi nikiwa uwanjani nikicheza, najisikia vizuri kucheza mashindano haya.

Shaffihdauda.co.tz: Nini matarajio ya kikosi kizima cha TP Mazembe kuelekea kwenye mchezo wenu dhidi ya Sanfrecce Hiroshima?

Samatta: Nafikiri wapinzani tumeshawaona wakicheza mechi ya kwanza na nadhani mwalimu atakuwa amejua matatizo yao, mapungufu yao na strength yao. Lakini kwa timu jinsi ninavyoiona watu wako vizuri na nadhani matarajio ni ushindi katika mchezo huo kwasababu tunayo hiyo nguvu katika mchezo uliopo mbele yetu.

Kwa upande wa ‘Drogba wa Dodoma’ Thomas Ulimwengu yeye hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kuelezea furaha aliyonayo kucheza mashindano hayo huku akisema ulimwengu utakuwa ukimwangalia Ulimwengu akifanya yake Japan.

Shaffihdauda.co.tz: Kuelekea mechi kati ya TP Mazembe dhdi ya Sanfrecce Hiroshima wewe binafsi upoje ki-saikolojia kuelekea kwenye mechi hiyo ambayo unaona ni kubwa kwa upande wako na nini matarajio yako?

Ulimwengu: Mimi najisikia furaha kuelekea mechi hiyo, lakini mimi binafsi nipo tayari na pia kama timu tupo tayari tunasubiri tu muda ufike na matarajio yangu ni kufanya vizuri katika mechi hiyo kwasababu ulimwengu mzima utakuwa unamwangalia Ulimwengu akicheza katika timu yake ya Mazembe. Kwahiyo najisikia furaha na natarajia kufanya mambo makubwa zaidi.

Ukitaka kushuhudia mechi hii live basi usikae mbali na StarTimes kwani wao pekee ndiyo watakufanya wewe ushuhudie mechi hiyo kali live lakini pia shaffihdauda.co.tz haitakuwa mbali, tembelea kila mara unavyoweza kupata updates za kila tukio litakalokuwa likijri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here