Home Kitaifa HIKI NDICHO ANACHOKITARAJIA SHAFFIH DAUDA KUTOKA KWA NAPE NNAUYE

HIKI NDICHO ANACHOKITARAJIA SHAFFIH DAUDA KUTOKA KWA NAPE NNAUYE

603
0
SHARE
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye

Jana Rais John Pombe Magufuli alitangaza baraza lake la mawaziri baada ya watu kusubiri kwa muda mrefu kusikia ni akina nani watapewa majukumu ya kusimamia wiara mbalimbali kwenye serikali ya wamu ya tano ambayo imeanza kwa kasi ya aina yake.

Kwenye upande wa michezo, Dr. Magufuli amemteuwa Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utaduni, Wasanii na Michezo. Wanamichezo wengi wanahitaji kuona Tanzania inafanya mabadiliko makubwa kaika nyanja ya michezo mbalimbali.

Swali linakuja, je Waziri Nape Nnauye atafanikiwa kuleta mabadiliko kwenye nyanja ya michezo akiwa ni kiungo kati ya serikali na viongozi wa vyama vya michezo hapa nchini ambapo kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa haifanyi vizuri katika mashindano ya kimataifa kwenye michezo husika?

Mchambuzi wa masuala ya michezo wa kituo cha Clouds Media Group Shaffih Dauda jana alisikika kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM akitaja matarajio yake kutoka kwa Waazriri huyo mpya aliyepewa majukumu ya kusimamia Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.

Dauda amesema yeye anategemea Nnauye atafanya utafiti kwa kushirikiana na wadau wa michezo ili kubaini changamoto zilizopo, kujua wapi pa kuanzia kuzitatua changamoto hizo zinazoikabili sekta ya michezo kwa muda mrefu.

“Kikubwa ambacho mimi nakitegemea kutoka kwake (Nape Nnauye) ni kutafuta wadau na kukutana nao kujua changamoto, kujua wapi pa kuingilia na kutokea halafu baadae akisha maliza hayo, ni kukubali kukaa katikati ya serikali na sekta ya michezo. Kama tulivyosikia kauli ya Rais akisisitiza ‘kutumbua majipu’ na huku kuna majipu mengi sana ambayo yanahitaji kutumbuliwa”, alisema Dauda wakati akitoa maoni yake juu ya kuteuliwa kwa Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.

“Kwahiyo yeye pia angaalie katika jicho hilo kwsababu hawezi kufanya kitu kama bado wale ambao wameingia ‘kimagumashi’ wataendelea na ataruhusu waendelee kuwepo au ataruhusu watu ambao hawana mchango waendelee kuingia kwenye sekta ya michezo”.

“Na hiyo inategemea na namna ambavyo yeye atakuwa anaichukulia sekta ya michezo, kama atakuwa anaona ni ya kawaida tu basi tutaendelea kubaki hivyohivyo, lakini kama ataichukulia kwa uzito wake naamini pia majipu mengi huku yatatumbuka”.

Wadau wengi wa michezo nchini wanasubiri kwa hamu kujua mipango ya kuhakikisha michezo hapa nchini inakuwa na tija na inakuwa na maendeleo siyo tu kwa taifa lakini pia kwa wanamichezo husika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here