Home Kitaifa AZAM MMEMSIKIA LAKINI ANACHOKISEMA MGOSI?

AZAM MMEMSIKIA LAKINI ANACHOKISEMA MGOSI?

497
0
SHARE
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi

Mnyama Simba baada ya kukamilisha mawindo yake visiwani Zanzibar, jana alirejea jijini Dares Salaam kwa ajili ya pambano lake la Ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC litakalosukumwa Jumamosi kwenye uwanja wa taifa.

Mussa Hassan Mgosi ni nahodha wa kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’ amewaahidi wapenzi wa Simba kuwa timu yao haitafungwa tena kwenye michezo ya ligi kuu na kwamba michezo miwili waliyopoteza hadi sasa inatosha ndani ya msimu huu.

“Tuashukuru mungu mpaka dakika hii mambo yanakwenda vizuri hakuna majeruhi kila mtu anamorali, kikbwa tuombe uzima katika mechi ya Jumamosi na mechi nyingine zinazokuja tumepanga tusifungwe”, amesema Mgosi.

“Sisi tumejiandaa kwa mechi zote zinazokuja mbele yetu ni kushinda kwasababu wapenzi wa Simba kila mmoja anatamani Simba msimu huu iweze kuwakilisha taifa kwenye michuano ya kimataifa na sisi wachezaji tunapigana kwa hali na mali ili tuweze kufanikisha hicho ambacho kila mtu anakitaka. Wachezaji wote tumeshakubaliana kwamba tumefungwa mechi mbili basi inatosha kwa msimu huu”.

“Wapenzi wa Simba watuombee tu, sisi tutawapa kile wanacho kisubiri kwa muda mrefu sasa”, alimaliza mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa bado hajafunga goli hata moja kwenye ligi inayoendelea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here