Home Kitaifa UNATAKA KUJUA KAMA OKWI ANAREJEA SIMBA AU LA? SIMBA IMEWEKA WAZI JAMBO...

UNATAKA KUJUA KAMA OKWI ANAREJEA SIMBA AU LA? SIMBA IMEWEKA WAZI JAMBO HILO

3363
0
SHARE

Okwi

Ndani ya siku mbili hizi imekuwa ikitajwa kuwa mchezaji nguli wa kimataifa wa Uganda ambaye aliwahi kutamba na klabu ya Simba SC Emanuel Okwi anarejea kujiunga na ‘wekundu wa Msimbazi’ katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili ili kuipa ‘tafu’ klabu hiyo katika harakati zake za kujaribu kutwaa ubingwa ambao imeukosa kwa miaka ya hivi karibuni.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya ‘mnyama’ Said Tuli ameweka wazi kuhusu taarifa hizo ambazo zimeenea kila kona lakini pia ametoa msimamo wa klabu juu ya suala la Okwi ambaye alitamba kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara.

“Suala hilo siwezi kulizungumzia kiundani kwasababu Okwi ni mcheaji wa timu nyingine na mchezaji ambaye anamkataba wa miaka mitano, kwahiyo si vizuri sisi kama viongozi wa klabu kuanza kuzungumzia habari za mchezaji ambaye anamkataba na timu nyingine”, amesema Tuli ili kutoa utata na mabishano yanayoendelea mtaani juu ya suala la nyota huyo kurejea Msimbazi.

“Kama kuna lolote au kama kuna kitu kitatokea klabu itatoa taarifa rasmi kupitia taratibu zetu za kawaida ambazo tunazitumia siku zote lakini sasahivi siwezi kusema kwamba Emanuel Okwi anakuja kuchezea Simba au kuna mipango yoyote inaendelea. Kiukweli sisi hatujui mpango wowote na tunaamini kwamba Okwi bado ananafasi ya kuendelea mbele huko ambako yupo”.

“Hatumuombei mabaya kwamba arudi tena kucheza soka huku, ni mchezaji mzuri amefanya mambo makubwa sana katika klabu ya Simba lakini pia sisi kama Simba tunajivunia kuona mchezaji kama huyo anazidi kwenda mbele zaidi kwahiyo nadhani tuzidi kumuombea azidi kwenda mbele zaidi kuliko kurudi Tanzania”

Emanuel Okwi ni mchezaji halali wa klabu ya SønderjyskE Fodbold inayoshiriki ligi ya nchini Denmark (Superliga) akiwa na mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo aliosaini mwaka huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here