Home Kimataifa LIVERPOOL YABANWA MBAVU, HII NDIYO HATMA YAKE MICHUANO YA EUROPA LEAGUE

LIVERPOOL YABANWA MBAVU, HII NDIYO HATMA YAKE MICHUANO YA EUROPA LEAGUE

507
0
SHARE

Liverpool-yafuzu

Liverpool imefanikiwa kumaliza hatua ya makundi ya Europa League ikiwa kinara wa kundi B kufuatia sare ya bila kufungana dhidi ya Sion mchezo uliopigwa kwenye dimba la Tourbillon .

Jurgen Klopp alianzasha kikosi ambacho kilicheza vizuri akiwepo Joerdan Henderson ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza chini ya Klopp tangu awe majeruhi kwa muda mrefu.

Kiungo mchezeshaji wa Liverpool Philippe Coutinho aliingia kipindi cha pili lakini hata hivyo mbrazil huyo hakusaidia kubadilisha matokeo kwani hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika timu zote zilitoka uwanjani bila kufungana.

Matokeo hayo yameipa nafasi Liverpool kusonga mbele ikiongoza kundi lake (Kundi B) huku Sion wakifuzu pia kwa hatua ya 32 bora wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Liverpool.

Draw kwa ajili ya ratiba ya 32 bora itafanyika Jumatatu December 14 mjini Nyon, Switzerland.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here