Home Ligi EPL HUYU NDIYE ‘KING OF ASSISTS’ WA EPL NA ULAYA, TAKWIMU ZINAZOMBEBA HIZI...

HUYU NDIYE ‘KING OF ASSISTS’ WA EPL NA ULAYA, TAKWIMU ZINAZOMBEBA HIZI HAPA…

540
0
SHARE

Mesut 1

Mashabiki wengi wa Arsenal wanafurahia kumuona namba 10 wao Mesut Ozil katika kiwango bora na hiyo inawafanya waamini kuwa msimu huu atakuwa kwenye orodha ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi ya England (PFA) na hata kuitwaa tuzo hiyo.

Kiwango alichokionesha Ozil kwenye mchezo dhidi ya Sunderland Jumamosi iliyopita kimezidi kumuongezea sifa mjerumani huyo ambaye kwasasa anaonekana ndiye mchezaji mwenye swagger ndani ya kikosi cha Arsenal kiwango ambacho hakukionesha wakati wa misimu yake miwili iliyopita.

Takwimu zilizotolewa na kituo cha Sky Sports zinazidi kuonesha ubora wa mshindi huyo wa kombe la dunia ukilinganisha na wachezaji wengine wa nafasi kama hiyo.

Ozil ndiye kinara wa assists na kutengeneza nafasi kwenye kikosi cha Arsenal ndani ya EPL pamoja na Ulaya kwa ujumla.

Kama striker wa Leicester City Jamie Vardy asingeivunja rekodi ya Rood van Nistelrooy basi Ozil asingekua na mpinzani katika kuwania tuzo ya PFA.

Hizi hapa ni takwimu za Mesut Ozil ‘The King of Assists’ zinazoonesha ubora wake ndani ya EPL na Ulaya.Mesut

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here