Home Kimataifa ZIFAHAMU REKODI MBALIMBALI ZA SERIE A ZILIZOTOKEA KATIKA RAUNDI YA 15?

ZIFAHAMU REKODI MBALIMBALI ZA SERIE A ZILIZOTOKEA KATIKA RAUNDI YA 15?

875
0
SHARE

Serie AMambo mengi yamejiri katika Ligi Kuu ya soka nchini Italia wikendi iliyopita.Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na rekodi ya Napoli ya kutofungwa kwa michezo 18 imevunjwa na klabu ya Bologna baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-2 katika uwanja wa Renato Dall’Ara.

Mara ya mwisho kwa kocha wa Napoli Maurizio Sarri kufungwa katika mchezo wa Serie A ilikuwa tarehe 23 mwezi wa Nane mwaka huu walipofungwa na Sassuolo kwa magoli 2-1.

Kwa mara ya pili msimu huu Gonzalo Higuain anafunga katika mechi nne mfululizo baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Bologna hapo jana.

higuainHiguain ana magoli 70 akiwa na jezi ya Napoli na hivyo kushika nafasi ya 9 ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Napoli akiwa sambamba na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo ambao ni Luis Vinicio na Faustinho Canè.

Nafasi ya kwanza ya ufungaji bora kwa klabu ya Napoli inashikiliwa na Diego Maradona ambaye amefunga magoli 115 katika michezo 259.

Kipa wa klabu ya Napoli Pepe Reina amecheza dakika 564 ugenini pasipokuruhusu wavu kutikiswa tangu afungwe magoli 2 katika mchezo wa sare ya magoli 2-2 dhidi ya Empoli.

Inter Milan wanazidi kuweka rekodi yao katika Ligi ya Italia kwani ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Genoa umeifanya klabu ya hiyo kucheza michezo 10 pasipokuruhusu goli lake kutikiswa katika michezo 15 ya Serie A msimu huu.

Mara ya mwisho kwa klabu ya Genoa kushinda mbele ya Inter Milan kwenye uwanja wa San Siro ilikuwa mwaka 1994 ambapo Genoa ilipata ushindi wa magoli 3-1.Wakati Inter wakiwa na rekodi nzuri ya kutoruhusu wavu wao kutikiswa,klabu ya Roma pia inazidi kujiwekea rekodi katika Ligi ya Italia hasa inapocheza na klabu ya Torino.

Sare ya goli 1-1 imeifanya klabu ya AS Roma kutokupoteza mchezo dhidi ya Torino tangu Torino wawafunge Roma mara ya mwisho 1990 katika ushindi wa goli 1-0.

Kocha wa Torino Giampiero Ventura naye hakuwa nyuma katika rekodi kwani katika mchezo dhidi ya AS Roma alikuwa anakaa katika benchi la Roma katika mchezo wa 193 na kuifikia rekodi ya kocha wa zamani wa Torino Gigi Radice.

Klabu ya Juventus imeweka rekodi ya kushinda michezo 5 mfululizo kwa mara ya kwanza tangu wafanye hivyo mwaka 2014.Juventus imepata ushindi wa michezo 6 kati ya 7 ya mashindano yote na kuweka rekodi ya kutoruhusu wavu wake kutikiswa kwa dakika 431.

Klabu ya Lazio haijawahi kuifunga klabu ya Juventus katika michezo ya nyumbani na ugenini ya Serie A tangu mwaka 2003 mwezi Desemba.

dybala 2Imefungwa michezo 16 na kutoka sare michezo 6.Mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala amefunga magoli 7 na kutoa asisti 3 katika raundi 15 za Serie A msimu huu sawa na Carlos Tevez wakati alipokuwa Juventus msimu uliopita.

Klabu ya Fiorentina haijafungwa katika michezo 8 ya kimashindano msimu huu ikiwepo ushindi wa michezo 5 na mingine ikitoka sare.

Fiorentina imepata penati 6 katika Serie A msimu huu zaidi ya timu nyingine zote za Serie A na kufanikiwa kufunga penati zote.
Sare ya bila kufungana ya Carpi na AC Milan ilikuwa ni sare ya 7 katika michezo 150 ya Serie A msimu huu.

Na mchezaji wa klabu ya Atalanta Giulio Migliaccio amekuwa mchezaji aliyetolewa kwa kadi nyekundu mapema kabisa katika Serie A ikiwa ni sekunde ya 32 dhidi ya Palermo.

Highlights

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here