Home Kimataifa WARRIORSS, WARRIORS WARRIORS…. STEPHEN CURRY.. WAMEITEKA NBA, ANATAFUTWA WA KUIKOMBOA.

WARRIORSS, WARRIORS WARRIORS…. STEPHEN CURRY.. WAMEITEKA NBA, ANATAFUTWA WA KUIKOMBOA.

564
0
SHARE

warriors

Katika mechi ya awali kati ya Golden State Warriors dhidi ya Brooklyn mambo hayakuwa shwari na ilikuwa ni moja ya mechi ambazo Warriors walikaribia kupoteza. Lakini kipindi hiki mambo yalikuwa tofauti kidogo na ushindi haukuwa mgumu hivyo na yote ikiwa ni uwezo wa kuamua mchezo wa mchezaji bora kwa sasa Stephen Curry.

Curry alifunga pointi 16 katika robo ya tatu kati ya pointi zake 28 za mchezo huo na Golden State Warriors kuibuka na ushindi wa pointi 114-98. Brooklyn walionekana kama wanaelekea kurudia yale ya mechi iliyopita kwani waliongoza kwa 75-70 zikiwa zimesalia dakika3:10 lakini kibao kiligeuka haraka.

Curry alifunga point 11 haraka haraka na kutoa pasi kwa Festus Ezeli na kupata pointi 15-4 wakati wanahitimisha robo ya tatu. Ghafla Brooklyn walijikuta nyuma katika dakika za mwanzo za robo ya nne kwa jumla ya pointi 96-85.

Kocha wa Brooklyn Nets, Lionel Hollins hakusita kumwagia sifa Stephen Curry katika mchezo huo. “Hivyo ndivyo namna ambayo wachezaji bora wanafanya na wanapaswa kuwa,’ alisema Holllins.

“Sio kila siku atafunga vikapu vingi kupindukia. Alifunga pointi 44 usiku uliopita, alifunga pia pointi 43 dhidi ya Charlotte siku mbili zilizopita. Haitaji kufunga sana, akiamua anafunga, akiamua pia anawapisha wenzake wafanye kwa niaba.”

Draymond Green alifunga pointi 22, pasi 7 na rebound 9 huku akiendelea kuwa na kiwango ambacho hapana shaka kitampa nafasi ya kushiriki katika mchezo wa All Star wa Februari. Klay Thompsonaliongeza pointi 21.

Thadeus Young alikuwa na pointi 25 na rebound 14 kwa upande wa Brooklyn Nets huku mchezaji Brook Lopez akifunga pointi 18. Brooklyn kabla ya huu mchezo walikuwa wameshinda michezo minne ya nyumbani hivyo kuvunjiwa mwendelezo wao.

REKODI

Warriors sasa wameshinda michezo 26 mfululizo pamoja na minne ya mwisho wa msimu uliopita hivyo wanahitaji ushindi mmoja kuwafikia Miami Heat ya msimu wa 2012-2013 kwa nafasi ya pili ya ushindi mfululizo.

Warriors wamefikia rekodi ya New York Knicks ya msimu wa 1969-70 ya kushinda michezo 12 mfululizo ya ugenini.

warCurry ameweza kufunga mtupo wa pointi 3 katika michezo 86 mfululizo, na anaweza kufungana kwa rekodi na Rashard Lewis aliyeweka kuanzia msimu wa 2007-09 kama atapata mtupo dhidi ya Indiana Pacers.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here