Home Ligi EPL Wayne Rooney katika Kiwango kibovu zaidi Maisha Mwake –  Mbinu za Van...

Wayne Rooney katika Kiwango kibovu zaidi Maisha Mwake –  Mbinu za Van Gaal zisivyomsaidia.

1566
0
SHARE

Katika kipindi cha maswali na majibu wiki iliyopita na gazeti moja nchini Uingereza – Wayne Rooney aliulizwa ikitokea amepewa nguvu za maajabu angependa kufanya nini.? Akajibu angependa kuwa na uwezo wa kumfanya ‘Asionekane’ mbele za watu.
Wiki iliyopita walipocheza vs Leicester, ndoto yake ya kutokutaka kuonekana ilipata ukamilifu kwa lugha ya kisoka – Alifichwa kabisa: Hakupiga shuti hata moja, hakutengeneza nafasi, hakupiga krosi, hakumpita mchezaji yoyote wa Leicester, hakufanya lolote la maana – alipiga pasi 23, kati ya hizo asilimia 70 tu ndio zilifika na ilipofika dakika ya 68 ya mchezo akatolewa katika mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1 @King Power Stadium.

Aina ya soka wanalocheza United hivi sasa chini Louis van Gaal ni tofauti kabisa na utamaduni wa klabu – soka lilopooza na kiukweli aina hii ya mchezo unaotokana na mbinu za LVG hazimsaidii kabisa Rooney.

 Rooney hakucheza jana vs West Ham na kuna uwezekano mkubwa asicheze katika mechi muhimu zaidi kwa United katika siku za hivi karibuni – dhidi ya Wolfsburg katika Champions League kutokana na majeruhi.

 

Wastani wa Rooney wa kupata goli katika mechi kwa unasomeka: katika kila dakika 525 anafunga goli moja, rekodi mbaya zaidi katika maisha yake ya soka. Tangu aanze kuitumikia United hajawahi kumaliza msimu wa EPL bila kufunga magoli zaidi ya 10, lakini mpaka sasa ana magoli 2, na zero assist – rekodi yake inaweza ikavunjika safari hii.

Baadhi ya watu wanadai kushuka huku kwa kiwango ni kutokana na umri wake, kwa umri wake wa miaka 30 ndani ha msimu wake wa 14 katika ligi ngumu zaidi duniani. Rooney alishacheza mechi 678 kabla ya birthday ya miaka 30 mnamo October 24 – idadi kubwa zaidi ya Ryan Giggs alipokuwa na umri huo – alicheza mechi 606. Idadi hii pekee inaonyesha kwamba amechoka.
  
Ukiangalia rekodi za wachezaji wanao-cover eneo kubwa la uwanja mpaka sasa kwenye EPL – Rooney bado yumo kwenye Top 5. Japokuwa anaelekea kutimiza mechi yake ya 700 hivi karibuni, anaonekana bado ana uwezo wa kinguvu kucheza soka la ushindani.

Kabla ya mechi ya Leicester, ni washambuliaji watatu tu ambao walikuwa wamekimbia dimbani kumzidi Rooney (73.98 miles) msimu huu – Harry Kane (80.1 miles), Jamie Vardy (77.34 miles) na Graziano Pelle (75.24 miles).

Tatizo ni, wenzake wote wanafunga, yeye hafungi, na kuna uwezekano mkubwa Rooney akawa anaanza mbele ya Kane na Vardy wakati wa Euro 2016 – hata akiendelea kuwa kwenye kiwango hiki.

Lakini angalau bado anajua yeye ni mchezaji wa nafasi gani katika kikosi cha England – mshambuliaji – tofauti na hali ilivyo Old Trafford.
 
Amekuwa akihamishwa kutoka nafasi moja mpaka nyingine na Van Gaal na hilo halijamsaidia Rooney.
Alijaribiwa kucheza namba 10 lakini LVG akamtoa na kuanza kuwachezesha kwenye nafasi hiyo Juan Mata, Ashley Young na Angel di Maria, miongoni mwa wengi. He Alipelekwa kucheza kwenye safu ya kiungo lakini klabu ikawasajili Morgan Schneiderlin na Bastian Schweinsteiger waliongezeka kwenye safu ya kiungo ambayo tayari ilikuwa na Ander Herrera, Michael Carrick na Daley Blind. Alitumika kama mshambuliaji mkuu mwanzoni mwa msimu lakini klabu ikawekeza kwa kumsajili Anthony Martial.

So, wapi atakapocheza Rooney? Mchezaji huyu hawezi kuhimili kucheza katika nafasi tofauti ndani ya mifumo tofauti, kama ambavyo Sir Alex Ferguson alivyoeleza katika Kitabu chake mwaka 2013.

Kuambiwa kucheza hapa na pale hakusaidii, pia inachangia United kucheza namna inavyocheza hivi sasa.

  

United wapo nafasi ya 4 kwenye ligi lakini wanashika nafasi ya 4 kwa timu zilizopiga mashuti machache langoni msimu huu – United 102, huku Sunderland (102), West Brom (99) are third in the table but have had the fourth fewest shots this season (102) with only Sunderland (101), West Brom (99) na Newcastle (95).

United hawatengenezi nafasi za kutosha.

Mesut Ozil  ametengeneza nafasi mara (58) – idadi kubwa zaidi katika Premier League, anayefuatia ni Dimitri Payet (47). Mchezaji wa United aliyetengeneza nafasi nyingi zaidi ni Mata ambaye ametengeneza mara 23, akifuatiwa na Rooney mara 12. Idadi ndogo zaidi kwa timu yenye ukubwa na wachezaji wa United.
Tatizo la United ni kucheza (sideways) wanaenda mbele na nyuma kwa kupiga pasi za kwenda pembe moja mpaka nyingine.
Rooney amepiga pasi 51 kwenda kwa Schweinsteiger msimu huu na 55 kwenda kwa Mata lakini amepiga pasi 17 tu kwenda Martial msimu huu – Martial ambaye hajafunga goli katika EPL tangu September 20, hili ni tatizo.

  
Rooney anapewa majukumu ya kumsapoti mshambuliaji – lakini yeye na Martial bado hawajaelewana, na yote yanatokana na kuwekwa mbalimbali uwanjani.

Alan Shearer aliliongelea hili vizuri katika uchambuzi wake kwenye kipindi cha Match of the Day: ‘Angalia nafasi iliyopo katikati yao washambuliaji. Hakuna namna nzuri ya kubadilishana nafasi kati ya Rooney na Martial, hawachezi kama pea. Hili linasababishwa na mbinu za kocha. Nisingetaka kabisa kucheza kwenye timu ya namna hii kwa sababu ya uchache wa nafasi wanazotengeneza.’

Rooney sio tena mchezaji ambaye anaweza kufunga magoli 20 na kuendelea kwa msimu, kama ilivyokuwa zamani – na kwa msimu huu hata kufikisha magoli 10 itakuwa jukumu zito kulifanikisha.
Hana wa kumlaumu zaidi yake mwenyewe na mbinu za Van Gaal lakini Rooney hajafanya jitihada za kumsaidia katika kipindi hiki kibaya – na inawezekana umefikia wakati wa kufunika mapazia ya maisha yake ya soka ndani ya Theatre of Dreams.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here