Home Kimataifa UKIMPINGA CURRY UMEUPINGA UKWELI. WARRIORS WANAPITA HATA JUU YA MOTO, WAENDELEA KUWEKA...

UKIMPINGA CURRY UMEUPINGA UKWELI. WARRIORS WANAPITA HATA JUU YA MOTO, WAENDELEA KUWEKA REKODI KALI.

559
0
SHARE

curry

Hesabu kwa vidole vya kiganja chako ni mara ngapi mchezaji kafunga pointi 40 msimu huu katika zaidi ya mara nne. Tizama pia mchezaji yupi anafunga sana kwa muda mchache. Usisahau kufungua fungua utambue nani anaongoza kwa kupata mitupo ya pointi tatu. Halafu weka orodha yako ya wafungaji bora msimu huu. Jibu ni stephen Curry.

Wakati mchezo wao dhidi ya Toronto Raptors ukibadilisha uongozi wa mchezo kwa zaidi ya ara sita katika robo ya nne peke yake ungeweza kujua ni kwa namna gani presha ipo migongoni mwa Golden State Warriors. Kila timu inatamani kuifunga Golden State Warriors na wao wanaonyesha kuwa muda wa kufungwa haujafika.

Stephen Curry alifunga pointi 44 alfajiri ya leo, huku akipata mitupo 9 ya pointi tatu kati ya mitupo 15 aliyojaribu, na kuifanya Warriors ifikishe michezo 21 mfululizo pasipo kupoteza tangu kuanza kwa msimuu huu. Warriors wameshinda kwa vikapu 112-109 dhidi ya Toronto Raptors.

Mpaka sasa Golden State Warriors wameshinda michezo 25 mfululizo kuanzia mwisho wa msimu uliopita. Hii inakuwa ni rekodi bora ya tatu katika NBA ya kushinda michezo mingi mfululizo nyuma ya Lakers ya msimu wa 1971-72 (33) na Miami Heat ya msimu wa 2012-2013 wao walishinda 27.

curr

Pamoja na kiwango bora cha Curry lakini Warriors ambayo inaonekana kwa kiasi kikubwa kumkosa Harrison Barnes inaonekana kuwa na muunganiko bora kabisa wa kitimu. Hata kocha wa muda Luke Walton sasa anaweza kujivunia namna ambavyo timu kwa ujumla inacheza kwa kumsikiliza na umakini mkubwa.

Thompson alifunga point 26 huku akimkaba vyema DeMar Derozan ambaye alifunga pointi 16 huku akipata mtupo mmoja katu ya kumi katika kipindi cha kwanza. Draymond Green alimaliza na pointi 16, rebound 9 na pasi 6 huku akiendelea kuwa mchezaji muhimu kupindukia na anayekomaa kila kukicha.

Kyle Lowry alifunga pointi 41 huku akipata mitupo 6 ya pointi tatu kwwa upande wa Toronto Raptors. Demar Derozan yeye alimaliza na pointi 16 katika moja ya siku ambayo uwepo wake uwanjani haukuwa mzuri dhidi ya ulinzi wa Klay Thompson. Toronto wamepoteza michezo 3 kati ya 4  ya mwisho.

Ushindi huu unaifanya Warriors kuivuka timu ya St. Louis Maroons kwa kushinda michezo mingi zaidi ya ufunguzi. Hivyo hakuna timu katika michezo minne yote inayotambulika Marekani kuwahi kushinda michezo 21 ya kwanza zaidi ya Warriors.

St. Louis Maroons ilikuwa inashiriki Union Association ambayo ndio Major League Baseball kwa sasa.

Toronto walimkumbuka Nelson Mandela katika mchezo huu huku pia kukiwa na wageni waalikwa kama Isiah Thomas na DIdier Drogaba.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here