Home Kimataifa MIAMI HEAT YA WADE YAIUNGUZA CLEVELAND CAVS. WADE ANG’AA LEBRON AKIWA NJE

MIAMI HEAT YA WADE YAIUNGUZA CLEVELAND CAVS. WADE ANG’AA LEBRON AKIWA NJE

444
0
SHARE

miami

Lebron yupo katika umri wa miaka 30 sasa, hana maisha marefu sana ya ubora wake katika NBA kama afya yake haitolindwa. Bahati nzuri sana hana urafiki wa karibu na majeraha. Ndio jambo ambalo kocha wake David Blatt hataki kumuona likimkuta kipindi hiki cha karibuni ambacho Cavs wanatamani kuwa mabingwa.

Dwayne Wade alifunga point 19 na kuiongoza timu yake ya Miami Heat kuibuka na ushindi wa vikapu 99-84 dhidi ya Cleveland Cavs iliyopoteza mcheo wake wa tatu mfululizo. Miami haikuonekana ikitetereka kabisa hasa ukizingatia mchezaji muhimu wa Cavs, Lebron James alipumzishwa katika mchezo huo.

Tyler Johnsoon aliifungia Miami point 19, mchezaji Gerald Green alifunga pointi 12. Goran Dragic aliongeza point 17 huku Chris Bosh akifunga pointi 14 dhidi ya Cleveland ambayo inaendelea kutizama hali ya mchezaji wao Kyrie Irving na uwezekano wa lini atarejea kutoka katika majeraha yake.

Kama ilivyo kawaida ya NBA, pamoja na mashabiki wa Heat kuwahi kumpenda na kulitaja vyema jina la Lebron wakati akiwachezea na kuwapa ubingwa mara mbili. Alfajiri ya Leo walisikika wakiimba kuwa “Lebron is tired”, yaani Lebron kachoka. Wakijaribu kudhihaki kitendo cha kupumzika au kupumzishwa.

Cavs walipoteza mchezo uliopita dhidi ya New Orleans Pelicans katika muda wa ziada huku Lebron akicheza dakika 45. Kocha wake akaona ni tija kumpumzisha. Richard Jefferson aliyeanza katika nafasi yake alifunga pointi 16, Smith alikuwa na 12, Jared Cunningham na Mathew Vellavedova walifunga 11 kila mmoja.

Hii ilikuwa mara ya nne kwa Cleveland kucheza bila Kyrie Irving na Lebron James kwa pamoja. Michezo yote hii Cavs imepoteza. Kevin Love alifunga pointi 5 huku akipata mitupo miwili pekee kati ya 11 aliyojaribu.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here