Home Ligi EPL MANCHESTER UNITED NA SAKATA KUHUSU NAFASI YA VAN GAAL

MANCHESTER UNITED NA SAKATA KUHUSU NAFASI YA VAN GAAL

429
0
SHARE

van gaal luis

Klabu ya Manchester United haina mpango wowote wa kuachana na kocha wao wa sasa Loius Van Gaal pamoja na kutopata matokeo mazuri uwanjani.

Gazeti la daily mail la chini England limeripoti kuwa klabu hiyo itaendelea kusalia na kocha huyo hadi mkataba wake utakapoishia 2017 na kisha kumuachia kijiti Ryan Giggs ambaye ni msaidizi wake hivi sasa.

Wiki hii kumekua na taarifa tofauti tofauti ndani na nje ya klabu kwamba huenda Manchester United ikawa katika mikakati ya kutafuta mbadala wa Louis Van Gaal huku yeye mwenyewe akisema ataondoka Manchester United endapo tu atakua kapoteza imani kwa wachezaji wake.

Pep Guadiola ambaye anakaribia kumaliza mkataba wake akiwa Bayern Munich mwisho wa msimu huu anatajwa kuitamani klabu hiyo huku pia kukiwa na tetesi za huenda Carlo Ancelotti akapewa dili la kuisongesha mbele klabu hiyo.

Wakati huo huo kocha Louis Van Gaal amesema haelewi kwanini mashabiki wamekua wakiimba ‘attack, attack, attack’ wakati Manchester United ni timu inayoshambulia kwani wamekua wakizitawala timu mwanzo hadi mwisho wa mchezo lakini akakiri tatizo kubwa la ufungaji magoli.

Manchester United inakabiriwa na mtihani mgumu Jumanne hii ambapo watatakiwa kushinda ugenini dhidi ya Vfl Wolfsburg ya Ujerumani katika uwanja wa Volkswagen Arena ili kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya, huku tayari ikitarajia kuwakosa nahodha Wayne Rooney, Morgan Schneiderlin na Paddy Macnair ambao ni majeruhi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here