Home Kimataifa NAPOLI ZAIDI YA ‘MAGUFULI’ NCHINI ITALIA

NAPOLI ZAIDI YA ‘MAGUFULI’ NCHINI ITALIA

609
0
SHARE
NAPLES, ITALY - DECEMBER 07: Goran Pandev of Napoli celebrates after scoring the goal 2-0 during the Serie A match between SSC Napoli and Udinese Calcio at Stadio San Paolo on December 7, 2013 in Naples, Italy. (Photo by Giuseppe Bellini/Getty Images)

NAPLES, ITALY - DECEMBER 07:  Goran Pandev of Napoli celebrates after scoring the goal 2-0 during the Serie A match between SSC Napoli and Udinese Calcio at Stadio San Paolo on December 7, 2013 in Naples, Italy.  (Photo by Giuseppe Bellini/Getty Images)

Na Simon Chimbo

Ni Napoli, Napoli, Napoli hivi sasa katika ligi kuu soka nchini Italia, Serie A. Klabu hiyo kwa mara ya kwanza imekaa juu ya msimamo wa ligi tangu walipofanya hivyo mwaka 1990 chini ya kocha Alberto Bigon waliposhinda ubingwa wao wa pili wa ligi hiyo maarufu ‘Scudetto’.

Kwa mara nyingine chini ya kocha Sarri, Napoli inaongoza tena ligi tangu ilipofanya hivyo miaka 25 iliyopita huku pia golikipa wake Pepe Reina akiweka rekodi ya kipekee baada ya kutoruhusu nyavu zake zitikiswe kwa dakika 533, na wakati huo huo mshambuliaji raia wa Argentina, Gonzalo Higuain akiwa amefunga magoli katika mechi zote nane mfululizo na magoli 12 katika michezo 14, ni kitu kikubwa sana.

Napoli pia hawajafungwa kwa kipindi cha dakika 743 huku wakifikisha mechi 7 bila kuruhusu goli, ni msimu adimu kwao na kitu kipya chini ya ualimu wa mwalimu Sarri.

Kocha wa sasa Maurizio Sarri hajapoteza michezo 18 mfululizo tangu alipofungwa na Sasuollo goli 2-1 mwezi Agosti siku ya ufunguzi wa ligi na kuvunja rekodi ya klabu yao waliyoiweka msimu wa mwaka 1989-90 na 2005-06. Tangu wapoteze na Sasuolo Napoli walipata ushindi katika michezo 14 mfululizo, wakitoa sare 4 huku wakifuga magoli 42 na kuruhusu magoli 8 tu golini kwao.

Rekodi aliyoiweka golikipa Pepe Reina katika klabu ya Napoli kutokufungwa goli katika kipindi cha dakika 533 ameipiku rekodi iliyokuwa inashikiriwa na golikipa wa Manchester United, David De Gea.

Kasi hii ya Napoli msimu huu nchini Italia, ya kurudia walichokifanya miaka ya 1989-90, inafananishwa na kasi hii ya nchini kwetu ya raisi John Pombe Magufuli ambapo watu wengi wanakumbuka zama za aliyekuwa rais wa kwanza Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere na waziri Waziri Mkuu wake wakati huo Moringe Sokoine.

Napoli sasa wana kazi moja muhimu ya kuipoka Juventus ubingwa waliochukua kwa misimu minne mfululizo na kama watafanya hivyo utakua ni ubingwa wao wa tatu katika historia ya klabu hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here