Home Kitaifa KIONGERA ATUA SIMBA, NA HILI NDIYO NENO LAKE LA KWANZA…

KIONGERA ATUA SIMBA, NA HILI NDIYO NENO LAKE LA KWANZA…

442
0
SHARE

Kiongera 1

Katika muendelezo wa kuboresha kikosi cha Simba, mchezaji Raphael Kiongera amewasili rasmi jana jioni katika kambi ya Simba visiwani Zanzibar.

Mshambuliaji huyu wa kimataifa amewasili visiwani Zanzibar akitokea Kenya ambapo alikuwa akiitumikia klabu ya KCB kama mchezaji aliyepelekwa kwa mkopo. Akiwa katika klabu ya KCB Kiongera aliweza kupigiwa kura na wapenzi wengi wa soka nchini humo na kuweza kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti.

Simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na Kiongera na kusema: “Nashukuru sana kwani ni furaha yangu kubwa sana kurudi tena katika klabu yangu ya Simba, ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa mashabiki na wapenzi wangu na hata wa soka la Tanzania kwa ujumla wategemee mambo mazuri kutoka kwangu”.

Chanzo: simbasports.co.tz

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here