Home Dauda TV DAUDA TV: GARY NEVILLE AISHUHUDIA VALENCIA IKIIBANA MBAVU BARCELONA

DAUDA TV: GARY NEVILLE AISHUHUDIA VALENCIA IKIIBANA MBAVU BARCELONA

517
0
SHARE

Valencia

Mabingwa watetezi wa taji la ligi ya Hispania na Ulaya Barcelona wamelazimihwa sare ya kufungana goli 1-1 na vigogo wengine wa ligi ya Hispania maarufu kama Spanish La Liga.

Valencia walijitahidi kuwazuia Barca wasipate bao na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa katika hilo katika kipindi chote cha kwanza na kwenda mapumziko huku timu zote zikiwa sare ya bila kufungana (0-0).

Bada ya kuona huenda Valencia ingelazima matokeo kubaki hivyo, Barcelona iliingia kipindi cha pili na kuanza kutafuta ushindi kwa lazima. Dakika ya 59 kipindi cha pili Luis Suarez akaipa Barca bao akimalizia kazi safi iliyofanywa na Lionel Messi.

Valencia 1

Wakati dakika zilizobaki ili mchezo huo kumalizika zikiwa zinahesabika, Santi Mina akawanyanyua mashabiki wa Valencia kwa goli lake la kusawazisha dakika ya 86 na kufanya matokeo kusomeka 1-1 na timu hizo kugawana pointi mojamoja.

Kocha mpya wa Valencia Garry Neville alikuwepo jukwaani akiwashuhudia vijana atakaonza kuwanoa siku chache zijazo walivyokuwa wakitoana jasho na Barcelona. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United ameteuliwa wiki hii kukiongoza kikosi hicho ambapo mchezo wake wa kwanza kama kocha utakuwa dhidi ya Lyon kwenye klabu bingwa Ulaya.

Valencia 2

Sare hiyo inamaanisha Barcelona inaendelea kushikilia usukani wa ligi kwa pointi 33 ikifuatiwa na Atletico Madrid huku Real Madrid ikiwa nafsi ya tatu kwa pointi 30.

Angalia video jinsi Barcelona ilivyojikuta ikilazimishwa sare na Valencia kwa kusawazishiwa goli lao dakika za jioni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here