Home Kimataifa Barca vs Valencia: Vita safu bora ya Ushambuliaji dhidi ya Safu bora...

Barca vs Valencia: Vita safu bora ya Ushambuliaji dhidi ya Safu bora ya Ulinzi

626
0
SHARE

Kikosi cha Luis  Enrique leo usiku kitasafiri mpaka kwenye dimba la Mestellah kuumana na Valencia ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa na hali tete, jambo lilopelekea kujiuzulu kwa kocha  Nuno Santo wiki hii na kuteuliwa kwa gwiji wa Manchester United Gary Neville kumrithi. 

  Mchambuzi wa zamani wa TV sasa anaungana na kaka yake Phil Neville ambaye atakuwa kwenye benchi la ufundi kwa pamoja kaimu kocha mkuu Salvador González Marco ‘Voro’, katika mechi ya leo na Barca, huku Gary akiwa jukwaani. 

  FC Barcelona wataingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na rekodi ya kushinda mechi zao 8 zilizopita katika kwenye mashindano yote.  Golikipa Marc-Andre ter Stegen amerejea kikosini baada ya kupona jeraha la goti. Jérémy Mathieu aliumia kwenye mechi ya Jumatano na ataukosa mchezo huo pamoja na Rafinha, Sergio Roberto na Douglas.  Kikosi kamili kipo hivi: Bravo, Piqué, Rakitic, Sergio, Dani Alves, Iniesta, Suárez, Messi, Neymar Jr, Mascherano, Bartra, Munir, Jordi Alba, Sandro, Adriano, Vermaelen and Samper.

  Valencia watawakosa wachezaji waonwasiopungua 10. Negredo, Orbán, André Gomes, Feghouli, Barragán, Alves, Rodrigo na Mustafi wote hawa watakuwa nje kwa majeruhi wakati Joao Cancelo na Javi Fuego wataukosa mchezo huo kutokana kuwa na kadi walizopata dhidi ya Sevilla katika dimba la Sánchez Pizjuán.

Safu kali vs Defensi Kali

  FC Barcelona wameshinda mechi zao zote 8 zilizopita hivi karibuni katika mashindano yote, wakifunga magoli 32 na wakiruhusu magoli manne tu katika mechi hizo. Vijana wa Luis Enrique wamefunga jumla ya magoli 33 katika ligi tu msimu huu, idadi kubwa kuliko timu yoyote, lakini Valencia ndio timu yenye rekodi nzuri sana ya safu ya ulinzi kwenye uwanja wao wa Mestallah, wakiwa hawapoteza mechi hata moja nyumbani, wakitoka sare 3 na wakishinda 3. 

Mtanange utakuwa live AzamTv kuanzi saa 4 usiku.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here