Home Kimataifa WADE AUWASHA MOTO, MIAMI HEAT YAILAMBA OKLAHOMA CITY THUNDER

WADE AUWASHA MOTO, MIAMI HEAT YAILAMBA OKLAHOMA CITY THUNDER

429
0
SHARE

wade

Ulitaka ladha ya playoff walau mapema na mwanzo kabisa mwa msimu? Basi kama ungetizama mchezo kati ya Miami dhidi ya Oklahoma City Thunder ungepata ladha hiyo pasi na shida yoyote ile kabisa. Moja ya michezo mizuri kuchezwa kwa siku za karibuni.

Dwayne Wade pamoja na kuwa na magoti mabovu lakini anabaki kuwa moja ya wachezaji bora kabisa kwa nafasi yake. Alifunga pointi 28 asubuhi ya leo huku ikiwa ni pamoja na mitupo huru miwili zikiwa zimesalia sekunde 1.5 na kuiongoza Miami kupata ushindi wa pointi 97-95.

Timu zote ziibadilishana uongozi mara 38 tofauti huku zikifungana ama kulingana kwa pointi mara 11.Ni nyingi zaidi kutokea msimu huu kwani mara nyingi zaidi ilikuwa mara 25. Wade tangu atue katika klabu ya Miami Heat hakuwahi pia kushuhudia hiki kwani mchezo uliotoa vingozi mara nyingi zaidi alioshiriki kabla ya huu ilikuwa mara 31.

“Kulikuwa na kila khali ama wingu la playoff katika mchezo huu, alisema Wde.” “Tuna kikosi kichanga ambacho wengi wao hawajahi kuwa na uzoefu na khali kama hizi, lakini ni jambo jema sana kuzishuhudia mapema hivi kwani zitawajenga.”

Chris Bosh alifunga point 16 na Goran Dragic aliongeza point 14 kwa Miami ambayo haijawa ile iliyozoeleka tena tangu aondoke Lebron James huku Wade na Bosh wakiwa wanaandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

RusselL Westbrook na Kevin Durant kila  mmoja alifunga point 25 katika mchezo huu.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here