Home Kimataifa ‘SKENDO FIFA’ U.S.A YAWAKAMATA MAAFISA 16 KWA RUSHWA

‘SKENDO FIFA’ U.S.A YAWAKAMATA MAAFISA 16 KWA RUSHWA

556
0
SHARE

fifa_web-jpg20150527101508

Maafisa 16 zaidi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, wanashikiliwa na shirika la kijasusi la Marekani FBI kwa skendo lukuki za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi, huku tayari raisi wa shirikisho hilo Sep Blatter na yule wa UEFA Michael Platini wakiwa kifungoni kwa siku 90.

Mwanasheria mkuu wa Marekani, Loreta Lynch amesema kuwa ukiukwaji wa haki na rushwa kamwe hautavumiliwa na kuwataka wote waliojihusisha na uchafu huo wa wizi wa mabilioni ya pesa kwa rushwa kujisalimisha wenyewe, kwani uchunguzi mkali unaendelea na kwamba wataweka wazi kila kitu.

Awali maafisa wa usalama wa Marekani, waliwashikilia marais wa mashirikisho ya soka ya CONCACAF na CONMBEL kwa skendo kubwa za wizi wa pesa za FIFA na kufanikisha dili chafu.

Aliyekua raisi wa shirikisho la soka la Brazil Ricardo Teixeira amekamatwa kwa uhalifu wa wizi wa dola milioni 200 za kimarekani huku raisi wa sasa naye wa shirikisho hilo la Brazil Marco Polo del Nero naye akishikiliwa kwa tuhuma hizo nzito.

Haya yote yalikuja baada ya maafisa wa usalama wa Uswisi na wale wa Marekani kushirikiana kutafuta ukweli juu ya kile kilichotawala juu ya upatikanaji wa nchi za kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 ambazo ni nchi za Urusi na Qatar.

Tayari shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limesema liko bega kwa bega na tayari kushirikiana na maafisa hao wa usalama kulisafisha shirikisho hilo ambalo hadi sasa limepoteza imani kwa wadau wa soka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here