Home Ligi BUNDESLIGA HUYU NDIYE MU-AFRIKA ANAYEWEKA HESHIMA UJERUMANI NA ULAYA, KESHO ANASHUKA UWANJANI UNAJUA...

HUYU NDIYE MU-AFRIKA ANAYEWEKA HESHIMA UJERUMANI NA ULAYA, KESHO ANASHUKA UWANJANI UNAJUA ATAFANYA NINI?

669
0
SHARE

Piere

  • Striker wa Borussia Dortmund Piere-Emerick Aubameyang amekuwa kwenye kiwango cha juu sana kwenye ligi ya Bundesliga msimu huu
  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon ameshatupia kambani magoli 17 ndani ya mechi 14 alizocheza hadi sasa
  • Aubameyang amefunga magoli hayo zaidi ya washambuliaji wengine kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar na Jamie Vardy

Jumamosi ya weekend hii kwenye ligi ya Bundesliga kutakuwa na mechi nyingi ambazo zitachezwa, lakini jicho la wengi litakuwa kwenye mchezo kati ya VfL Wolfsburg dhidi ya Borussia Dortmund hasa kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Piere-Emerick Aubameyang kutaka kujua atafanya nini kwenye mchezo huo kutokana na kuwa na rekodi nzuri ya kufunga msimu huu.

Aubameyang amekuwa gumzo kwenye ligi ya Bundesliga na barani Ulaya kutokana na moto alionao tangu kuanza kwa ligi hiyo ya Ujerumani, je kesho Aubameyang ataendelea kuwatesa magolikipa wa ligi hiyo kwa kupasia nyavu? Majibu ya maswali yote yatajibiwa baada ya dakika 90 za mchezo huo kukatika ndani ya uwanja wa Volkswagen Arena.

Piere 2

Striker wa Leicester City Jamie Vardy ndiyo mshambuliaji hatari zaidi kwenye ligi ya Uingereza msimu huu hadi sasa akiwa amefunga magoli 14 kwenye mechi 14 alizocheza, lakini Ujerumani wao wanamshambuliaji hatari zadi pengine hata ya Vardy.

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Piere-Emerick Aubameyang tayari yeye ameshatumbukia nyavuni mara 17 katika michezo 14 ambayo amecheza hadi sasa na kuisaidia timu yake kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga nyuma ya vinara wa ligi hiyo Bayern Munich.

Wakati Vardy anavunja rekodi ya striker wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy kwa kufunga mechi 11 mfululizo, Aubameyang alikuwa anatwaa tuzo ya heshima baada ya kufanikiwa kufunga mabao mengi kwenye mechi 14 tangu Gerd Muller alipofanya hivyo kwa kufunga mabao 19 kwenye mechi 14 kwenye msimu wa mwaka 1976-77.

Piere 1

Raia huyo wa Gabon amecheza kwa dakika  1226 hadi sasa msimu huu akifanikiwa kupiga jumla ya mashuti 55 katika harakati zake za kutaka kupasia nyavu huku akiwa ni mwiba mchungu kwenye safu za ulinzi za timu pinzani.

Matokeo mazuri yanamaanisha Aubameyang siyo tu amefunga zaidi ya mshambuliaji mwingine ambaye yupo kwenye kiwango kizuri kwa sasa msimu huu Jarmie Vardy, lakini pia Neymar, Lionel Mesi, Luis Suarez, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Robert Lewandowski pamoja na Gonzalo Higuain hawajaweza kufanya hivyo. Na hiyo inamaanisha Aubameyang ndiye mshambuliaji mwenye moto mkali barani Ulaya kwa sasa.

Usishangae kusikia anatajwa kwenye tetesi za kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili mwezi January, Liverpool ni moja ya klabu zinazotajwa kumuhitaji mchezaji huyu ili akaungane na kocha wake wa zamani Jurgen Klopp.

Hapa unaweza kujionea mwenyewe takwimu za Aubameyang zikionesha ni kwa jinsi gani na namna gani striker huyu alivyo na uchu pindi alitazamapo lango la timu pinzani.

Piere 3

Piere 4

Wolfsburg vs Borussia Dortmund, Preview

Ni mechi kati ya vikosi viwili vyenye majina makubwa kwenye ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, VfL Wolfsburg ikiwa inapointi 25 wakati Borussia Dortmund yenyewe inaponti 32, timu hizi zinafatana kwenye msimamo wa ligi, Dortmund ikiwa nafasi ya pili huku Wolfsburg ikikaa kwenye nafasi ya tatu.

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Volkswagen Arena Jumamosi ya December 5, Wolfsburg wakiwa wenyeji wa pambano hilo.

Wolfsburg itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare tasa kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ambayo inashikilia mkia FC Augsburg kwenye uwanja wa SGL Arena weekend iliyopita.

Sare hiyo ilitokana na uwezo mkubwa uliooneshwa na magolikipa wa timu zote mbili kufanya kazi ya ziada kuzinusuru timu zao mbele ya mashabiki zaidi ya 27,000.

Kikosi cha Borussia Dortmund chenyewe kilipata ushindi mnono wa goli 4-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani Signal Iduna Park dhidi ya Stuttgart siku ya Jumamosi iliyopita.

Kama kawaida yake Aubameyang akarudi kambani mara mbili dakika ya 19 na dakika ya 90 kiungo Gonzalo Castro alifunga dakika ya tatu wakati mlinzi wa Stuttgart Georg Niedermeier alijifunga dakika ya 65 kukamilisha ushindi wa Dortmund wa goli 4-1.

Goli pekee la kufutia machozi kwa upande wa Stuttgart lilifungwa na kiungo Daniel David dakika ya 40 ya mchezo huo.

Matokeo yanayobashiriwa kwenye mchezo huo ni Dortmund kuibuka na ushindi wa bao 2-0. Kikosi cha kocha Thomas Tuchel kinatarajiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu ngumu.

Vikosi vinavyotarajiwa:

Wolfsburg (mfumo ni 4-4-2): Benaglio; Trasch, Naldo, Dante, Schafer; Vieirinha, Guilavogui, Arnold, Schurrle; Dost, Kruse

Borussia Dortmund (mfumo ni 4-3-3): Burki; Piszczek, Papastathopoulos, Bender, Schmelzer; Castro, Gundogan, Kagawa; Mkhitaryan, Aubameyang, Reus.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here