Home Kimataifa Benitez hali tete – Madrid waondolewa Copa Del Rey kwa uzembe wake

Benitez hali tete – Madrid waondolewa Copa Del Rey kwa uzembe wake

481
0
SHARE

Wakati kukiwa na presha ya kuhakikisha timu yake inapata matokeo chanya, baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika La Liga, Hali inazidi kuwa tete kwa kocha Rafael Benitez baada ya maamuzi yake katika upangaji wa kikosi kuiponza Madrid kuondolewa katika michuano ya Copa Del Rey.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la AS, miamba hiyo ya La Liga, imeondolewa kwenye Copa Del Rey baada ya kumchezesha mchezaji aliyefungiwa Dennis Cheryshev katika mechi ya michuano hiyo dhidi ya timu ya daraja la pili Cadiz, jumatano iliyopita.

  Cheryshev alifunga goli la kwanza katika mechi ya ushindi vs Cadiz kabla ya kutolewa baada ya Madrid kuwaambiwa walikuwa wamecheza ‘blunder’ kumchezesha Cheryshev ambaye alikuwa na kadi – ambazo alipata wakati akiwa kwa mkopo Villareal, hata hivyo Madrid wamejitetea kwamba hawakuwa wamepewa taarifa juu ya zuio hilo kwa mchezaji wao – lakini Fransico Rubio, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya soka Hispania amegoma kusikiliza utetezi huo wa Madrid.

Madrid pia wanaamini kwamba mchezaji husika ilibidi ataarifiwe juu ya kufungiwa kwake kabla ya mchezo na sasa inaonekana wazi klabu hiyo itakata rufaa juu ya uamuzi huo baada ya Raisi wa klabu hiyo Florentino Pérez alisema jana kwamba wanaangalia uwezekano wowote wa kisheria ili kesi hiyo washinde.

Uamuzi huu wa kamati ya mashindano umezidi kumeongezea presha kocha Rafael Benitez ambaye wadau wengi wamekuwa wakimlaumu kwa uamuzi wa kunchezesha Cheryshev bila kuangalia kama hakuwa na shida yoyote.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here