Home Kimataifa KIBIBI KIZEE ANARUDI INGAWA KWA KUJIKONGOJA

KIBIBI KIZEE ANARUDI INGAWA KWA KUJIKONGOJA

594
0
SHARE

JuventusNi wazi kuwa kuwa Serie A inaendelea kuimarika kila kukicha kutokana na ushindani unaooneshwa na timu kubwa pamoja na timu nyingine zinazoshiriki Ligi hiyo.
Timu kubwa hapa nazungumzia Juventus,Napoli,Inter Milan huku kukiwa na hali ya kusuasua kwa timu za AC Milan,Fiorentina na AS Roma.

Timu za kawaida ambazo zinafanya vziuri mpaka sasa ni pamoja na Sassuolo,Torino na Atalanta.Kabla ya kuanza kwa msimu, watu wengi waliipa nafasi klabu ya Juventus kutetea ubingwa wake.

Lakini kadiri muda unavyokwenda, timu hiyo inaonekana kuwakatisha tamaa watu walioipa nafasi kutokana na matokeo yake ya kusuasua katika baadhi ya michezo ya Serie A.

Kama unakumbuka wakati Ligi inaanza,Juventus walipoteza michezo miwili ya mwanzo dhidi ya Udinese nyumbani na dhidi ya AS Roma ugenini.

Mechi dhidi ya Udinese ilikuwa ni mechi ya kwanza ya msimu huu wa Serie A kwa Juventus kucheza pasipokuwa na nyota wake kama Arturo Vidal,Andrea Pirlo na Carlos Tevez huku Claudio Marchisio akiwa ni majeruhi.

Hakuna shaka wachezaji hao wamefanya kwa kiasi kikubwa Juventus kuanza kwa kusuasua katika Ligi ya Italia.Habari njema ni kuwa wachezaji wapya wameanza kuonesha uwezo wao na kuifanya Juventus ianze kupata matokeo.

Nyota kama Paulo Dybala,Juan Cuadrado,Mario Mandzukic,Alex Snadro na Mario Lemina wanaanza kuonesha thamani zao kwa Bianconeri na kuwathibitishia mashabiki wa Juventus kuwa Kibibi Kizee kinarudi katika makali yake.

Kiuhalisia Juventus ilikuwa inakosa uwiano mzuri wa maneneo yote matatu ndani ya uwanja.Maeneo hayo ni pamoja na idara ya ulinzi,idara ya kiungo na idara ya ushambuliaji kucheza pasipokuwa na maelewano.

Ni ngumu kutengeneza muunganiko wa timu kwa mwezi siku,wiki au mmoja bali huchukua muda na ni kitu ambacho Allegri anakifanya kwa sasa kwa kutengeneza uwiano bora kwa timu yake.

Juventus inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 24 tofauti ya pointi 7 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya kwanza ya Napoli yenye pointi 31.Hii ina maana ya kuwa klabu ya Juventus au waweza kuiita ‘Kibibi Kizee cha Turin’ inajikongoja kurudi katika makali yake.

Faida kubwa waliyonayo Juventus ambayo inaweza kuwafanya wakatetea taji lao ni kuwa bado wana kikosi cha wachezaji wenye uzoefu mkubwa ambao wanaweza kuhimili presha ya Ligi ya Italia na kujua mahitaji ya Ligi pindi timu inapokuwa katika wakati mgumu kama walionao sasa.

Uwepo wa wachezaji wakongwe katika timu hiyo kama nahodha wa timu Gianluigi Buffon,Giorgio Chiellini,Claudio Marchisio,Stephen Lichtsteiner na Patrice Evra ni silaha tosha ya wao kutetea ubingwa wao.

Bado ni mapema sana kusema kuwa bingwa anaweza kuwa Napoli,Inter Milan au Fiorentina kwani bado kuna michezo 24 imebaki kuamua bingwa wa Serie A msimu huu.

Ambacho nakiona kocha wa Juventus Massilimiliano Allegri anapaswa kufanya kwa sasa ni kuhakikisha kuwa anawapa nafasi baadhi ya wachezaji vijana kama Daniele Rugani, Andrea Favilli pamoja na Mattia Vitalli ili kuwapa nafasi ya kupumzika baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ambao wanaonesha dalili za kuchoka.

Giorgio Chiellin,Buffon,Barzagli wanahitaji kupata muda wa kupumzika hasa katika michezo ambayo haina presha kubwa ili kuendelea kuwaweka fiti katika michezo migumu ya timu hiyo.
Bado naamini Bainconeri wanaweza kutoa ushindani kwa vilabu vya Napoli,Inter Milan na Fiorentina ambao wanafanya vizuri kwa sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here