Home Kimataifa WESLEY MATHEWS AREJEA NYUMBANI ASHANGILIWA, DALLAS YAWALAMBA PORTLAND TRAIL BLAZERS

WESLEY MATHEWS AREJEA NYUMBANI ASHANGILIWA, DALLAS YAWALAMBA PORTLAND TRAIL BLAZERS

522
0
SHARE

dallsJambo kubwa la kwanza kwenye mchezo huu ilikuwa ni Wesley Matthews kuonekana kukubaliwa na kushangiliwa katika kurejea kwake. Kisha ikabidi afurahie ushindi walioupata.

Matthews alirejea Portland kwa mara ya kwanza tangu kusainiwa na klabu ya Dallas kama mchezaji huru na kuiongoza Mavericks kuishinda timu yake ya zamani ya Portland Trail Blazers 115-112 katika muda wa ziada Jumanne usiku na alfajiri ya Jumatano kwa huku Afrika Mashariki.

“Sisi ni timu kongwe na hapana shaka tumecheza vyema na ni wazuri, hivyo ilikuwa rahisi tu kubadilika kiasi na kurekebisha kiwango chetu kwa khali ya juu na kuulinda ushindi mkubwa tuliouhitaji,” alisema Matthews. Mathews alimaliza mchezo na pointi 18 lakini alipata kushangiliwa sana na mashaiki wake wa zamani hao.

Deron Williams alifunga point zake nyingi zaidi msimu huu 30, na Dirk Nowitzki akaongeza point 28 na kuisadia Dallas Mavericks kuvunja muendelezo wa kufungwa ambao ulifika michezo 5.

Lillard aliweza kumaliza na pointi 25, pasi 10 na rebounds nane. Meyers Leonard alikuwa na pointi 23 na wachezaji wa benchi la Portland waliweza kuwafunika wale wa akiba wa Dalls kwa kufunga pointi 73-16.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here