Home Kimataifa KOBE AREJEA NYUMBANI KULIKOMLEA KUAGA LAKINI ACHAPWA, AHUENI YA KWANZA KWA PHILDELPHIA...

KOBE AREJEA NYUMBANI KULIKOMLEA KUAGA LAKINI ACHAPWA, AHUENI YA KWANZA KWA PHILDELPHIA 76ERS

603
0
SHARE

kobe

Wakati Warriors wakishikilia rekodi ya kutokufungwa mpaka sasa, wenzao Philadelphia 76ers walikuwa wakishikilia rekodi ya kutokushinda mpaka walipokutana na ndugu zao L.A Lakers ambao nao walikuwa miongoni mwa waliokuwa na rekodi mbovu ya kutokupata ushindi.

Philadelphia 76ers walikuwa na rekodi ya kutokushinda michezo 18 yote ya mwanzo huku pia wakiwa na rekodi ya timu zote zinazoshiriki mashindano mbalimbali chini Marekani ya kutokushinda katika michezo 28 mfululizo, hii ikiwa kuanzia mwisho wa msimu uliopita.

Macho na masikio ya kila mtu uwanjani yalikuwa kwa Kobe Bryant. Bryant alikuwa anarejea kwao, nyumbani kabisa achilia Los Angeles ambako alikuwa anatafutia mkate wake kunako klabu ya L.A Lakers. Lakini 76ers hawakujali hilo, walihitaji ushindi wao wa kwanza na wakaupata kwa kushinda 103-91.

Bryant akikumbatiwa na legend wa Dixers Sonny Hill kwa hisia kubwa
Bryant akikumbatiwa na legend wa Dixers Sonny Hill kwa hisia kubwa

Hivyo klabu ya Sixers inabaki ikifungana na New Jersey Nets (sasa Brooklyn Nets) iliyoanza pia kwa kufungwa michezo 18 mfululizo msimu wa 2009-2010. Hii ni rekodi mbovu zaidi katika NBA kwa timu kuanza bila kuonja ushindi.

Tofauti na siku zote ambapo huu ulikuwa uwanja ambao alizomewamara nyingi, Kobe Bryant muda wote alisikia kelele za KOBE, KOBE, KOBE kutoka jukwaani. Hata muda aliopata mitupo yake mitatu ukumbi uliwaka kwa kuimba M-V-P.

bryant

Kobe anakiri hakutegemea kupokelewa vile huku akikiri kuwa wachezaji wengi wa Sixers walikuwa watoto wakati yeye anaanza maisha yake ya mchezo wa kikapu na katika NBA.

bryantkb

Kobe alipewa jezi ya shule aliyosomea ya Lower Merion high school na kocha wake wa kipindi hicho Gregg Downer aliyeambatana na moja ya wachezaji wanaoheshimika katika klabu hiyo na NBA kwa ujumla Julius Erving maarufu kama Dr. J.

BRYA

 

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here