Home Kimataifa Dalili za CR7 kuondoka Bernabeu zazidi kuongezeka: Awatibua Madrid kwa jambo hili

Dalili za CR7 kuondoka Bernabeu zazidi kuongezeka: Awatibua Madrid kwa jambo hili

769
0
SHARE

Wakati tetesi za kuondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu huu zikizidi kushika hatamu kwa mchezaji Cristiano Ronaldo, klabu yake ya Real Madrid imekasirishwa na tabia mpya aliyoianzisha nahodha huyo wa Ureno.

 Inaripotiwa kwamba Real Madrid wamekasirishwa na tabia mpya ya Ronaldo kusafiri mara kwa mara kwenda barani Afrika katika nchi ya Morocco kukutana na rafiki yake Badri Hari.

 Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Ronaldo amekuwa akitumia muda wake wa kupumzika jioni kwenda Morocco kukutana na bingwa wa kickboxer, Badr Hari jijini Rabat Morocco – mji ambao upo kaskazini mwa Morocco.

Baada ya mazoezi kila siku jioni, Ronaldo anaripotiwa kuchukua ndege yake binafsi yenye thamani ya €19m kupaa juu ya bahari ya Atlantic kwenda kukutana na rafiki yake kisha kurejea jijini Madrid kwa mazoezi siku inayofuatia.

 Mabosi wa Real wanapata wasiwasi na tabia hiyo ya Robaldo na wanahisi inachangia katika kushusha kiwango cha Ronaldo msimu huu.

Baada ya Nahodha wa Ureno kufanya trips nyingi kwenda Morocco mwezi uliopita, picha nyingi za Hari na Ronaldo zilipostiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Vyombo vingi vya habari nchini Hispania vimekuwa vikiuponda urafiki wa Ronaldo na Hari – gazeti la El Mundo limeuelezea uhusiano huo kama ‘controversial’ na huku wakimtuhumu Mmorrocco huyo amekuwa akitishia watu na ni mgomvi ambaye muda mwingine huwaingia watu maungoni.

 Badr Hari ana uraia wa nchi mbili, alizaliwa Uholanzi na ni mmoja ya watu maarufu zaidi katika dunia ya kickboxing. Ana rekodi ya kucheza mechi 118 na kupoteza 12 tu.

Mabosi wa Real Madrid watakuwa wanaombea uhusiano huu upungue nguvu na Ronaldo apunguze au kuacha kabisa kwenda Morocco na kuweka umakini wake kwennye kazi yake. Ikiwa hili litaendelea na kiwango chake kikibaki kuwa hapa kilipo basi uhamisho wa mwanasoka huyo mwishoni mwa msimu ndio utakuwa suluhisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here