Home Ligi BUNDESLIGA HUU NDIO MSIMAMO WA DORTMUND KUHUSU MAHUSIANO YAO NA JURGEN KLOPP

HUU NDIO MSIMAMO WA DORTMUND KUHUSU MAHUSIANO YAO NA JURGEN KLOPP

510
0
SHARE

Borussia-Dortmund-Press-Conference

Klabu ya soka ya Borrusia Dortmund imesema kuwa haitaharibu mahusiano yao mazuri na kocha Jurgen Klopp wa Liverpool hata kama kocha huyo atataka kuwasajili wachezaji wa klabu yao ya Dortmund.

Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Borrusia Dortmund, Hans-Joachim amesema hakuna tatizo wala pingamizi lolote kwa kocha huyo kutaka kuwasajili wachezaji wa klabu yao ilimradi tu afauate utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwasiliana kwanza na klabu kabla ya kuwasiliana na mchezaji.

Aidha klabu ya Borrusia Dortmund kupitia kwa mkurugenzi wake huyo imesema wanajisikia faraja kutokana na kuanza vizuri katika maisha yake mapya Anfield huku akisema kamwe hawataharibu mahusiano yao na kwamba Klopp ataendelea kuwa sehemu muhimu katika historia ya klabu yao.

Jurgen Klopp ambaye aliwapa ubingwa wa Bundesliga klabu ya Borrusia Dortmund mara mbili na kuifikisha fainali ya klabu bingwa Ulaya msimu wa mwaka 2013 amesisitiza taarifa za kwamba kuna vikwazo vya yeye kuwasajili wachezaji kutokea Dortmund sio za kweli na kwamba mahusiano yake na Dortmund ni ya afya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here