Home Kitaifa AZAM FC KUCHEZA NA MGAMBO, AFRICAN SPORTS KABLA YA KUWAVAA SIMBA SC

AZAM FC KUCHEZA NA MGAMBO, AFRICAN SPORTS KABLA YA KUWAVAA SIMBA SC

582
0
SHARE
Kikosi cha Azam FC kilichocheza dhidi ya JKT Ruvu
Kikosi cha Azam FC kilichocheza dhidi ya JKT Ruvu
Kikosi cha Azam FC

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC Jumatano hii wanataraji kusafiri hadi Mkoani Tanga kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa ligi kuu Bara tarehe 12 mwezi huu dhidi ya Simba SC. Ikiwa Tanga, Azam itacheza michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya timu nyingine za ligi kuu.

“Tunataraji kwenda Tanga Jumatano hii kwa ziara ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara. Tutacheza mechi mbili, dhidi ya JKT Mgambo siku ya Alhamis kisha tutacheza na African Sports siku ya Jumamosi” amesema msemaji wa mabingwa hao wa ligi kuu bara msimu wa 2013/14.

Azam FC inashikilia usukani wa ligi kuu ikiwa na alama 25 baada kucheza michezo tisa itawavaa Simba katika mchezo unaotaraji kuwa na upinzani mkali. Simba tayari wameelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiweka ‘fit’ kwa mchezo huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here