Home Kimataifa PAU GASOL ATUMA SALAMU KWA KOBE BRYANT, ACHEZA VYEMA CHICAGO IKIWABOMOA SAN...

PAU GASOL ATUMA SALAMU KWA KOBE BRYANT, ACHEZA VYEMA CHICAGO IKIWABOMOA SAN ANTONIO

470
0
SHARE

bullsUkiwa na kikosi kama Chicago Bulls unahitaji kila mchezaji awe tayari kuchukua majukumu na kubeba timu. Huwezi kuwa tegemezi kwa Jimmy Butler siku zote kuwa atakuwa katika ubora wake. Ndicho alichofanya Paul Gasol dhidi ya San Antonio Spurs alfajiri ya leo.

Paul Gasol alifunga pointi 18 huku akidaka rebound 13 na kupiga block ya maana dhidi ya Lamarcus Aldridge ambaye bado anatafuta namna ya kufanya aliyokuwa akiyafanya na Portland katika klabu yake hii mpya.

Lakini wakati Paul Gasol akifanya hayo kwa ubora wachezaji wengine hawakuwa nyuma kwani Jimmy Butler aliongeza pointi 14, Joakhim Noah akafunga pointi 8, pasi 7 na Rebound 11. Mchezaji wa akiba Doug Mcdermott aliongeza pointi 12. Derick Rose alifunga pointi 11 na pasi 6.

Spurs walipata chance ya mwisho ya kuweza kufungana na Chicago ama kushinda lakini majaribio ya pointi 3 kutoka kwa Kawhi Leonard na Tony Parker yote yaliangukia pua.

Kawhi Leonard alifunga pointi 25 na kumaliza na rebound 8, Lmarcus Aldridge alimaliza na pointi 21 na rebund 12 huku Tony Parker akimaliza na POinti 13. San Antonio Spurs walikuwa wameshinda michezo 9 kati ya 10 iliyopita.

KOBE ATAJWA TENA

Mchezaji Pau Gasol hakusita kumsifia Kobe Bryant huku akimataka kuwa mwenye furaha katika kipindi hiki kilichobaki na acheze kwa amani kabisa huku akifurahia kila anachofanya.

JOAKHIM NOAH JE?

Joakhim Noah alicheza mchezo wake wa 557 akimpita Dave Dorzine katika nafasi ya tisa ya wachezaji waliocheza michezo mingi zaidi na klabu ya Bulls.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here