Home Kimataifa MWEWE WAITAFUNA RADI… ATLANTA HAWKS YAIFUMUA OKLAHOMA CITY THUNDER

MWEWE WAITAFUNA RADI… ATLANTA HAWKS YAIFUMUA OKLAHOMA CITY THUNDER

548
0
SHARE

kd

Kuna wakati mchezaji hufungi lakini ulinzi wako unakuwa msingi wa mafanikio kwa klabu yako. Ndiyo yamekuwa maisha ya mchezaji Thabo Sepholosha kwa muda mrefu sasa.Mtu muhimu pale timu yake inapohitaji mkabaji hasa.

Hakufunga alfajiri ya leo dhidi ya klabu yake ya zamani ya  Oklahoma City Thunder lakini alidaka rebound8 akatoa pasi 6 na kupokonya mipira mara 4.

Jeff Teague moja ya point guards wazuri lakini wanaokumbana na wingi wa point guards wenye uwezo na wanaopewa umakini kuliko yeye alimaliza mchezo na point 25. Atlanta Hawks ikapata ushindi wa pointi 106-100 dhidi ya Oklahoma City Thunder. Oklahoma imeshuhudia rekodi yao ya kushinda michezo minne ikivunjwa.

Millsap alifunga pointi 26 na kudaka rebound 11 na kuiongoza Atlanta iliyokuwa katika kiwango kizuri kwa usiku wa kuamkia leo. Al Hoford aliongeza point 21 na rebound 13.

Kevin Durant alimaliza na point 25 katika mchezo huo huku ukiwa ni mchezo wa kwanza Oklahoma wanapoteza tangu arejee kutoka katika majeruhi ya wiki chache zilizopita.

Rusell Westbrook aliiongoza Oklahoma kwa kufunga pointi 34, rebound 11 na pasi 7. Serge Ibaka alikuwa na point 17 huku yeye na Durant wakimaliza na block 4 kila mmoja.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here