Home Kimataifa Jana Usiku Zimetolewa tuzo za La Liga: Messi, Ronaldo, Neymar wachuana tena

Jana Usiku Zimetolewa tuzo za La Liga: Messi, Ronaldo, Neymar wachuana tena

1087
0
SHARE

Baada ya jana mchana kutajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia, wanasoka walioingia kwenye Top 3 ya tuzo hiyo, Messi, Ronaldo na Neymar usiku wa jana walipambana tena katika tuzo za La Liga.

  
Lionel Messi alitajwa kuwa mchezaji bora wa La Liga msimu uliopita mbele ya Ronaldo katika tuzo hizo zilizofanyika huko Barcelona.

Baada ya kuiongoza Barca kushinda treble msimu uliopita, Luis Enrique nae akatajwa kuwa mshindi wa tuzo ya kocha bora.

Messi kwa mara nyingine tena akatajwa kuwa mshindi wa tuzo mshambuliaji bora – hii ikiwa mara ya sita kushinda tuzo za uchezaji na ushambuliaji bora wa La Liga.

  Neymar ambaye nae kwa mara ya kwanza ameingia kwenye top 3 ya Ballon D’or alitajwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka Amerika.

  Golikipa wa Barca, Claudio Bravo akashinda tuzo ya golikipa bora, huku kiungo wa Valencia Sofiane Feghouli akishinda tuzo ya mwanasoka bora kutoka Afrika.

  Cristiano Ronaldo hakutoka kapa – akashinda tuzo ya mashabiki (5 Star Player Award), huku Sergio Ramos akishinda tuzo ya beki bora na Tuzo ya kiungo bora ikienda kwa James Rodriguez.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here