Home Kitaifa ILE MOVIE KATI YA SIMBA NA AZAM IMEMALIZIKA NA MSHINDI KAPATIKANA

ILE MOVIE KATI YA SIMBA NA AZAM IMEMALIZIKA NA MSHINDI KAPATIKANA

750
0
SHARE

Simba vs URA 9

Ile movie iliyokuwa ikichezwa kati ya klabu ya Simba na Azam FC zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara imeshamalizika huku klabu ya Simba ikifanikiwa kumtwaa starling wa movie hiyo ambaye ni mchezaji wa kiganda Brian Majwega.

Vilabu hivyo ambavyo miezi michache iliyopita vilikuwa kwenye vita nyingine ya kumuwania mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ huku Simba ikidai mchezaji huyo bado alikuwa anamkataba na klabu yao lakini Azam ilimnasa baada ya mkataba huo kuvunjwa na TFF na Messi kusajiliwa na Azam kama mchezaji huru.

Safari hii kibao kilihamia kwa ‘waoka mikate na watengeneza ice cream’ ambao nao kwa wakati tofauti waliingia mgogoro na mchezaji wao Brian Majwega baada ya mchezaji huyo kusugua benchi kwa muda mrefu hali iliyopelekea aamue kutimkia zake kwao Uganda na aliporejea nchini akaomba kufanya mazoezi na kikosi cha Msimbazi.

Baada ya kocha wa Simba Dylan Kerr kuvutiwa na mchezaji huyo ndipo mishemishe za kumsajili zikaanza lakini Azam waliposhtukia dili hilo wakatangaza kuwa bado wanamkataba na mchezaji huyo na kwamba alitoroka na kuacha kazi yake kwenye timu hiyo na endapo Simba wakimsajili basi wao watawachukulia hatua.

Brian Majwega akiwa ndani ya jezi ya Azam FC
Brian Majwega akiwa ndani ya jezi ya Azam FC

Jana viongozi wa pande zote mbili wakakutana ili kuzungumzia sakata hilo na wakafikia makubaliano kwamba mchezaji huyo apewe ruhusa ya kuvaa uzi mweupe na mwekundu na kuanza kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam.

Ili kupata uhakika zaidi mtandao huu ukamtafuta afisa habari wa Azam FC Bw. Jafar Idd ili athibitishe taarifa za Azam kutoa baraka zake kwa mchezaji huyo kujiunga na ‘mnyama’ naye bila hiana akaweka mambo hadharani.

“Brian Majwega alikuwa na mkatba halali na klabu ya Azam lakinin tunashukuru viongozi wa Simba wamekuwa waungwana na wametumia busara baada ya kujua ni kweli mchezaji huyo anamkataba na Azam walichokifanya ni kurudi chini na kuamua kuja kwenye meza ya mazungumzo na Azam”, amesema msemaji wa Azam Jafar Idd.

Mjwega akiwa ndani ya uzi wa Simba baada ya kuomba kufanya mazoezi na kikosi hicho hivi karibuni
Mjwega akiwa ndani ya uzi wa Simba baada ya kuomba kufanya mazoezi na kikosi hicho hivi karibuni

“Taratibu zilianza jana kati ya viongozi wa Simba pamoja na viongozi wa Azam na kwamba hivisasa Brian Majwega ni mchezaji halali wa Simba baada ya Simba kutumia uungwana wa kukaa chini na Azam na kuzungumza suala hili kwenye taratibu zinazokubalika za mpira tumelimaliza na tumempa ruhusa Majwega kwenda kucheza Simba”.

Majwega alisafiri na kikosi cha Simba ambacho kipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu inayotarajiwa kuendelea December 12, 2015 ambapo siku hiyo Simba itacheza dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here