Home Kimataifa GRIFFIN ANG’AA, DEANDRE JORDAN NOMA. CLIPPERS YAIKALISHA VIBAYA PORTLAND

GRIFFIN ANG’AA, DEANDRE JORDAN NOMA. CLIPPERS YAIKALISHA VIBAYA PORTLAND

490
0
SHARE

GRIFFIN

Blake Griffin akiwa vyema na Deandre Jordan akiamka salama basi siku hiyo mpinzani huwa na wakati mgumu sana. Ni ngumu kumzuia Griffin asifunge kwa sasa huku ni changamoto kushindana na Jordan kudaka rebounds akiwa katulia siku hiyo.L.A clippers yashinda 102-87 dhidi ya Portland Trail Blazers.

Blake Griffin alimaliza na pointi 23 huku akidaka rebound 8 akiingia katika mchezo huu na rekodi bora ya wastani wa mitupo aliyopata katika NBA. Deandre Jordan yeye alimaliza mchezo akiwa na rebound zake nyingi zaidi kwa msimu huu 24, huku akiongeza pointi 18.

Chris Paul alicheza kwa dakika 24 tu huku akiondoka uwanjani akiwa na pointi 10 na pasi 6. Alishindwa kuendelea na mchezo kwa kile kinachoonekana kuwa na majeraha ya misuli ya upande wa mbavu.

Griffin amefunga point 450 ambazo ni nyingi zaidi kuwahi kufungwa na mchezaji yoyote wa Clippers katika michezo 18 ya mwanzo. Hii ni tangu L.A Clippers walivyohama kutoka SAn Diego na kuhamia Los Angeles msimu wa mwaka 1984-85.

Maurice Harkless aliiongoza Portland akiwa na pointi 15 . CJ McCollum , ambaye aliingia akiwa wa pili katika timu kwa wastani wa pointi 20.4 kwamchezo, alikosa mitupo nane kati ya tisa ya mwanzo na kumaliza akipata mitupo 4 kati ya 15 huku akiwa na pointi 12 na pasi 10.

Damiarn Lillard ameanza michezo yote 264 ya michezo ya ligi akiwa na Portland tangu ajiunge na timu hiyo miaka minne iliyopita huu akiwa katika msimu wake wa kwanza wa dili la $120m. Aliumia katika mchezo huu na kama akikosa mchezo unaofuata dhidi ya Dallas rekodi yake ndio itavunjika rasmi.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here