Home Kimataifa Top 3 ya Ballon D’or kuwagharimu Barcelona Bil. 5 – sababu hii...

Top 3 ya Ballon D’or kuwagharimu Barcelona Bil. 5 – sababu hii hapa

493
0
SHARE

Katika biashara yoyote unayoifanya katika ulimwengu huu kuna vitu vya aina mbili: Hasara na faida. Katika biashara ya usajili ya kumsajili Neymar Dos Santos, klabu ya FC Barcelona imepata mafanikio makubwa ya kutwaa vikombe vitatu msimu uliopita, lakini taarifa iliyotoka mchana wa leo juu ya jina la mshambuliaji kuwemo kwenye top 3 ya wachezaji wanaogombea tuzo ya Ballon D’or itawaingiza Barcelona hasara ya mabilioni ya fedha.

 

 Uwepo wa jina la Neymar katika Top 3 ya Ballon D’Or utaigharimu Barcelona kiasi cha €2m – zaidi ya Billioni 5 za Kitanzania – kwa majibu wa makubaliano ya Barca na Santos wakati wakifanya biashara ya Neymar.

Mbrazil huyo anaungana na Muargentina Lionel Messi kushindana na Cristiano Ronaldo kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia.

 Neymar alijiunga na Barcelona katika dili lenye thamani ya €57.1m kutoka Santos mnamo June 2013 lakini kwenye dili hilo kulikuwepo na kipengele kinachowalazimisha Barca kuongeza kiasi cha €2m endapo tu Mbrazil huyo angeimgia kwenye Top 3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here