Home Kimataifa ROCKETS WAPENYEA KWENYE TUNDU DOGO, WAICHAPA NEW YORK KNICKS. BADO HAWAJAWA VIZURI

ROCKETS WAPENYEA KWENYE TUNDU DOGO, WAICHAPA NEW YORK KNICKS. BADO HAWAJAWA VIZURI

548
0
SHARE

HOUS

James Harden aliiongoza Houston Rockets akimaliza mchezo akiwa na  pointi 26 . Thornton na Clint Capela kila mmoja alikuwa na pointi  18 na  Trevor Arizaa akamaliza na 16. Houston ikashinda 116-111 dhidi ya New York Knicks.

Arron Afflalo alikuwa na pointi 31 kwa Knicks , ambayo ilicheza bila mfungaji wao bora na anayeongoza katika klabu hiyo  Carmelo Anthony kwa sababu ya ugonjwa . Kristaps Porzingis aliongeza pointi 20 na 13 rebound.

Houston Rockets, baada ya kufunga pointi nne za mwanzo wa mchezo na kuongoza, hawakuweza kuongoza tena mpaka ulipofika muda wa ziada yaani overtime.

“Ilikuwa ni somo katika uvumilivu wetu,” alisema kocha wa muda JB Bickerstaff . “Hatukuanza vizuri mchezo huu, lakini tulitulia na kuukabili mchezo kama ulivyo na hili ni jambo la kuwapongeza wachezaji wetu kwa ushupavu wa akili na ujasiri. ”

Houston Rockets wameendelea kucheza kwa kusuasua tangu kuanza kwa msimu, na iliwabidi kutoka nyuma kwa pointi 14 katika robo ya 4 ya mchezo na kuja kufungana kwa point baada ya Thornton kupata mtupo wa point 3 zikiwa zimesalia sekunde 32.

” Kasi ya mchezo iliongezeka,” kocha wa Knicks Derek Fisher alisema. ” NBA ina michezo mirefu  na tulikuwa na baadhi ya turnovers ambazo hazikuwa na maana au ulazima wa kutokea. Wao ndipo wakapata nafasi ya kutushambulia kwa kubadilishana vyema na tukashindwa kuwazuia na kuhimili katika robo ya nne . ”

Howard aliongeza pointi 14 na Capela alikuwa 11 na rebound kwa Rockets.

Thomas alimaliza na pointi 15, Kevin Seraphin alikuwa 14 na Williams aliongeza 12 kwa Knicks .

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here