Home Kimataifa Ni marufuku kusajili mchezaji wa Kituruki – Russia, kisa hiki hapa.

Ni marufuku kusajili mchezaji wa Kituruki – Russia, kisa hiki hapa.

640
0
SHARE

Vilabu vya nchini Russia vimepigwa marufuku rasmi kusajili mchezaji wa aina yoyote kutoka klabu za Uturuki kuanzia dirisha la usajili la mwezi January 2016.

 Katazo hilo limetolewa na serikali ya Russia katika kipindi ambacho nchi za Urusi na Uturuki zipo katika msuguano mzito wa kisiasa.

Msuguano umetokana na ndege ya kivita ya Urusi kutunguliwa na vikosi vya Uturuki katika mpaka wa nchi hiyo na Syria Jumanne iliyopita, tukio ambalo lilichukua maisha ya rubani wakati mtu mwingine alipona na kuokolewa na wanajeshi waliokuwa katika opereshenj maalum.

Kutokana na tukio hilo, Russian imewawekea vikwazo vya kiuchumi Uturuki, vikwazo ambavyo pia vinahusisha biashara ya usajili wa wachezaji baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko aliiambia R-Sport news agency: “Ikiwa mtu yoyote anataka kusajili mchezaji kutoka Uturuki, hakutokua na uwezekano huo.”

Hata hivyo, aliongeza wachezaji wenye asili ya kituruki ambao wamekuwa wakicheza Urusi hawatohusika na katazo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here