Home Kimataifa Je, Inter itafanikiwa kuuvunja mfupa wa Napoli uliodumu kwa miaka 18 sasa.

Je, Inter itafanikiwa kuuvunja mfupa wa Napoli uliodumu kwa miaka 18 sasa.

519
0
SHARE

nn

Usiku wa leo Napoli itawakaribisha Inter kwenye mchezo mgumu wa Serie A kwenye dimba la San Paolo huko kusini mwa nchi ya Italia katika mji wa Napoli.

Inter maarufu kama Nerazzurri ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 30 mbili zaidi ya Inter inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 28. Timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa na rekodi nzuri ya kushinda michezo yao miwili iliyopita, Napoli ilipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini mbele ya Hellas-Verona wakati Inter iliitandika nyumbani timu ngeni kwenye Serie A Frosinone mabao 4-1.

Mpambano huu utazikutanisha timu mbili zenye safu kali ya ulinzi kwenye Serie A msimu huu. Inter mpaka sasa imeruhusu mabao saba tu na pia imecheza mechi nne zilizopita bila kuruhusu nyavu zake kuguswa. Wapinzani wao Napoli wamefungwa jumla ya mabao nane tu huku wakiwa wamezuia nyavu zao kuguswa katika mechi tano zilizopita.

Msimu uliopita kwenye michezo yote miwili ya Serie A hakuna timu iliyofanikiwa kumfunga mwenzie, mechi zote mbili ziliisha kwa sare ya mabao 2-2 .Mara ya mwisho Inter kuifunga Napoli ilikuwa ni mwezi December mwaka 2012 ,Inter ilishinda mabao 2-1 kwa mabao ya Freddy Guarin na Diego Milito kwenye dimba la Giuseppe Meazza.

Pia imepita karibia miaka 18 tangu Inter ipate ushindi kwenye dimba la San Paolo. Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1997, Inter ilishinda 2-0 kwa mabao ya Fabio Galante na bao la kujifunga la Francesco Turrisi.

Kama una king’amuzi cha Startimes basi kazi kwako imeisha kwasababu ikifika saa 2 kamili usiku tune to channel ya World Football uone mechi hii live

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here