Home Kimataifa GRIFFIN AINGIE KWENYE MBIO ZA MVP? AENDELEA KUWA NA KIWANGO BORRA, CLIPPERS...

GRIFFIN AINGIE KWENYE MBIO ZA MVP? AENDELEA KUWA NA KIWANGO BORRA, CLIPPERS IKIICHAPA MINNESOTA TIMBERWOLVES.

575
0
SHARE

GRIF

Griffin alifunga 12 ya pointi zake 26 katika dakika 6:32 za mwisho, akadaka rebound  nane na na kusaidia pasi saba na kuiongoza klabu yake ya Los Angeles Clippers kuibuka na ushindi wa 107-99 dhidi ya Minnesota Timberwolves.

Los Angeles Clippers wameshinda mchezo wao wa pili mfululizo ikiwa ni baada ya kushinda mchezo wao uliopita dhidi ya New Orleans Pelicans. Hii inakuwa mara ya kwanza kushinda mfululizo tangu washinde michezo minne ya mwanzo mfululizo ya kufungua msimu huu.

“Siyo kila mara mambo huenda vyema ndani ya uwanja, lakini tunatakiwa kucheza vyema tupate ushndi  hasa katika kanda hii ya Magharibi ,” alisema Chris Paul , ambaye alikuwa na pointi 20 na kusaidia pasi tisa . “Timu imejitahidi kufanya kila kitu kwa ufasaha hasa kupata mitupo tuliyokuwa tukirusha.”

Clippers waliweza kupata asilimia 52 ya mitupo yao. Hii inamaanisha kuwa mpaka sasa wameshinda michezo 49 mfululizo ikitokea wamepata asilimia 50 au zaidi ya mitupo yao waliyojaribu.

J.J. Redick alifunga pointi 18 huku Clippers ikiwapiga Minnesota kwa mara ya 13 mfululizo wakati ikiwa ni mara ya saba mfululizo katika uwanja wa Staples Center.

Timberwolves walipata ushindi wa mwisho  dhidi  ya Clippers ilikuwa Machi 5 , 2012, wakati Kevin Love ambaye kwa sasa yupo Cleveland Cavaliers alipofunga pointi 39 na 17 rebounds katika ushindi wa 95-94 kwenye uwanja wa Target Center.

Andrew Wiggins alifunga pointi 21 kwa Wolves , ambayo ilikuwa imeshinda  michezo yao ya awali mitatu . Karl- Anthony Towns, alikuwa na pointi 17 na rebounds nane.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here