Home Kitaifa ZANZIBAR MWENYEJI MICHUANO YA KAGAME 2016

ZANZIBAR MWENYEJI MICHUANO YA KAGAME 2016

638
0
SHARE

ZFA

Na Abubakar Kisandu, Zanzibar

Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kimethibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya vilabu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati KAGAME CUP, ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi wa July, 2015.

Mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Massoud Attai amethibitisha kuwa Zanzibar watakuwa wenyeji kuandaa mashindano hayo ambapo walipelekea maombi yao kwa CECAFA kwa kutaka kuwa wenyeji na CECAFA wamekubali Zanzibar kuandaa michuano hiyo mwakani (2016) na kwasasa maandalizi yameshaanza maana Baraza la michezo tayari wameshapokea barua ya kuwa Zanzibar ni wenyeji wa michuano hiyo.

“Ni kweli Zanzibar tumepeleka maombi yetu kwa CECAFA kuwa mwenyeji na tayari wameshatukubalia, kwaiyo yatafanyika mwakani bila wasiwasi wowote”, amesema Attai.

Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika ndani ya visiwa vya zanziabar ambapo timu ya Mafunzo na JKU ndiyo bingwa na makamu bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2014-2015 ndio watakaowakilisha Zanzibar, lakini pia hii si mara ya kwanza kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambapo waliwahi kuwa wenyeji miaka mingi sana kama mwaka 1985 na 1990 na mashindano yakachezwa kwa utulivu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here