Home Kimataifa PACERS WANA MOTO MKALI, PAUL GEORGE HASHIKIKI. INDIANA PACERS YAIFUMUA CHICAGO

PACERS WANA MOTO MKALI, PAUL GEORGE HASHIKIKI. INDIANA PACERS YAIFUMUA CHICAGO

456
0
SHARE

pac

Baada ya kuvunjika mguu katika maandalizi ya timu yake ya taifa, hakuna aliyejua majaaliwa ya Paul George tena. Wakati wengi wakiamini hatokuwa yule tena aliyezoeleka, khali imekuwa tofauti kwani amerudi moto na kila anachogusa ni dhahabu kwa wakati huu.

Paul George alifunga pointi 33 na kuondoka na rebound 8 akiisaidia Pacers kuipiga timu ngumu ya Chicago Bulls kwa jumla ya vikapu 104-92. Na sasa Indiana Pacers ipo katika kiwango bora ajabu hasa baada ya kuondokewa na wachezaji wake muhimu David West na Roy Hibbert.

Monta Ellis alifunga point 14, George Hill alimaliza na pasi 10 na rebound 10 huku sasa Indiana pacers ikiwa na rekodi nzuri 10-5. C.J Miles alimaliza na point 16.

Nikola Mirotic alifunga point zake nyingi zaidi kwa msimu huu, 25 huku Jimmy Butler ambaye ndiye mchezaji bora wa Bulls kwa sasa akiwa na pointi 16. Chicago Bulls ambayo ilianza msimu vyema sasa ina rekodi ya 9-5.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here