Home Kitaifa TFF kwanini inabariki sajili kama hizi.? Simba SC wapewe adhabu kwa usajili...

TFF kwanini inabariki sajili kama hizi.? Simba SC wapewe adhabu kwa usajili wa Majwega, JKT Ruvu iadhibiwe kwa Dilunga

490
0
SHARE

tffd

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
KUNA mambo yanafanyika Tanzania tu, na yanakubalika haraka. Kuanzia kwa viongozi wa juu, wachezaji hadi kwa mashabiki hufurahia baadhi ya mambo kishabiki sana. Mathalani, usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Uganda, Brian Majwega.

Mchezaji huyu ana mkataba na klabu ya Azam FC lakini sasa anafanya mazoezi na klabu ya Simba SC ambayo inadai imemsaini. Utamsaini vipi mchezaji wa timu nyingine.? Hivi, TFF inashindwa kusimamia sheria zake na kuwachukulia hatua Simba.?

Haya ni mambo ya kizamani sana. Nachofahamu mimi ni makosa makubwa kiongozi wa klabu kuzungumza moja kwa moja na mchezaji wa timu nyingine ambaye yuko ndani ya mkataba na klabu yake.

JKT Ruvu wamefanya hivyo kwa kiungo mshambulizi wa Stand United, Hassan Dilunga. Stand bado wana mkataba na Dilunga lakini cha kusikitisha hakuna kiongozi wa JKT Ruvu ambaye aliwafuata Stand kwa nia/lengo la kumsaini, Dilunga.

Matokeo yake mchezaji mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wa JKT Ruvu wamefanikisha usajili wa mchezaji huyo na si ajabu TFF ikaupitisha na Dilunga akaichezea JKT Ruvu mara baada ya ligi kuu kuanza upya baada ya kusimama kwa muda.

Msimu uliopita mshambulizi raia wa Mexico, Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliichezea Real Madrid kwa mkataba wa mkopo akitokea Manchester United. Mara baada ya kumalizika kwa msimu, Hernandez akarejea zake United ili kuwalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliokuwa umesalia.

Klabu ya Bayer 04 Leverkursen ilimsaini baada ya kufikia makubaliano na klabu yake ya Manchester United. Si, Hernandez na Leverkusen ndiyo waliokutana kwanza ili kufanikisha usajili huo, bali ni viongozi wa United na wale wa timu hiyo ya Ujerumani ndiyo walikaa na kufikia muafaka wa kuuziana mchezaji huyo. Mpira wa kulipwa unaongowa kwa weledi.

Kwa hili la Simba na Majwega, Dilunga na JKT Ruvu inaonesha wazi kuwa -hakuna-u-proo wowote na Tanzania itachukua muda sana kuingia katika mpira wa kulipwa. Daniel Lyanga, unaweza kujua chanzo cha mshambuliaji huyo kushindwa kuichezea Simba hadi sasa.? FC Lupopo ya DR Congo ndiyo timu halali ya Lyanga.

Kilichotekea ni kwamba. Baadhi ya ‘Mafionso-Genge la Wahuni’ waliamini wanaweza ‘kuipiga changa la macho’ timu hiyo ya DR Congo na Simba ikamtumia mchezaji huyo bila tatizo. Lakini wote wamekwama, Lyanga na Simba hawakuhakikisha suala la usajili huo linakamilika kwa kufuata sheria za uhamisho wa wachezaji.

Mchezaji si proo, na viongozi waliofanikisha uwepo wake Simba hawana upeo wowote kuhusu mpira wa kulipwa ndiyo maana hawakuwahi kuzungumza na viongozi wa timu hiyo ya DRC na kutokana na ‘umbumbu’ wao.

Kabla ya kumuitaji mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine kwanza unapaswa kuzungumza na timu yake. Kinyume chake ni makosa na kwa nchi zilizoendelea hatua kali za kinidhamu huambatana na adhabu. Ashley Cole na Jose Mourinho ‘ walibamwa’ na wakaadhibiwa baada ya Mourinho kujaribu kutumia mbinu mbaya kumuhamisha Cole kutoka Arsenal mwaka 2005.

Azam FC wasikubali kirahisi kudharauliwa, Stand wana haki ya kuendelea kuzuia usajili wa Dilunga JKT Ruvu, na je, TFF huwa inabariki sajili kama hizi kwa sababu gani? Simba ipewe adhabu, labda na kwa JKT Ruvu na timu nyingine zinazojaribu kukiuka kanuni na taratibu za uhamisho wa wachezaji wenye mikataba na timu nyingine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here