Home Kimataifa LEBRON JAMES ATIA REKODI, CLEVELAND CAVALIERS YATIWA KIBINDONI NA TORONTO RAPTORS

LEBRON JAMES ATIA REKODI, CLEVELAND CAVALIERS YATIWA KIBINDONI NA TORONTO RAPTORS

535
0
SHARE

LEBRON

Kyle Lowry alifunga pointi 27 na Demar DeRozan aliongeza 20 kwa upande wa Toronto  Raptors na kuiongoza  kuwapiga Cleveland Cavaliers 103-99 alfajiri ya Alhamis  kwa ushindi wao wa tatu mfululizo.

LeBron James alikuwa na pointi 24, pasi nane  na rebounds sita kwa Cavaliers ( 11-4 ) , ambao walipoteza mchezo wao wa tatu mfululizo  wakiwa nje ya uwanja wa nyumbani . Kevin Love aliongeza pointi 21 na 13 rebounds.

“Wana timu nzuri na bora sana, Love alisema. Sisi pia tumekuwa na kikosi kwa ujumla tumekuwa tukicheza vizuri. Tumejaribu kufanya mbinu ambazo ndio huwa msingi wetu, tumetupa mitupo kama siku zote na kilichotokea mwisho ni kile ambacho wengi huwa hawapendi kukiona kikiwakuta”.

“Nadhani uchovu ulicheza ama kutawala sehemu kubwa katika hilo,” kocha wa Cleveland David Blatt alisema.

“Nadhani tumecheza tukiwa na khali ya uchovu , na hii ni kwa sababu za wazi . Tuko pungufu sana na nguvu ya timu kwa ujumla inatetereka kwa kiasi kikubwa sana. Wachezaji wetu walicheza kwa bidii. Naamini ulifika muda wachezaji wakaishiwa nishati, sio utetezi ila ni jambo jepesi la kiuchunguzi. ”

Cavs inaendelea  kucheza bila wachezaji wake majeruhi  Kyrie Irving , Timofey Mozgov , Mathew Dellavedova na Iman Shumpert , lakini James alikataa mapendekezo ya uchovu kuwa ndio ilikuwa sababu.

“Siyo jambo la utetezi, ” alisema. “Tunahitaji kushikilia kila mmoja na kuwajibika zaidi. “Tunachotakiwa kufanya ni  kucheza vizuri, na tutafanya hivyo. Lakini sidhani kama tulicheza vyema na kwa mwendo uliozoeleka usiku wa leo. ”

LEBRON AENDELEA KUKWEA KILELE CHA MAFANIKIO

Lebron kushoto mwenye jezi nyeupe akiwa Cleveland, Miller kulia akiwa na Indiana Pacers
Lebron kushoto mwenye jezi nyeupe akiwa Cleveland, Miller kulia akiwa na Indiana Pacers

Lebron James aliweza  kumpita mchezaji wa zamani wa Indiana Pacers na moja ya shooters bora kuwahi kukanyaga ligi ya NBA,  Reggie Miller katika nafasi ya 18 ya orodha ya NBA kwa ufungaji wa pointi nyingi zaidi za muda wote. Akiwa na pointi zake 24, James sasa ana pointi 25298 katika maisha yake ya NBA.

HIGHLIGHTS

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here