Home Kimataifa CLIPPERS WAPOTEZA FUNGUO, SASA WANAFUNGWA MFULULIZO. WAAMBULIA KICHAPO DHIDI YA UTAH...

CLIPPERS WAPOTEZA FUNGUO, SASA WANAFUNGWA MFULULIZO. WAAMBULIA KICHAPO DHIDI YA UTAH JAZZ

460
0
SHARE

CLIP

Sio kila siku ambayo huja kama bahati mbaya kwako dhidi ya mpinzani wako fulani. Huwadia  siku ambayo utampatia tu achilia mbali ubabe anaoweza kuwa nao.

Hii ndio kauli unayoweza kuitumia kwa mchezaji Gordon Hayward ambaye hakuwahi kupata ushindi dhidi ya Los Angeles Clippers kwa takribani miaka 4. Siku hiyo iliwadia ambayo ilikuwa nzuri sana kwake kwani aliongoza mauaji kwa mikono yake mwenyewe.

Alinyanyua mikono akajipigapiga kisha akapiga kelele za kujihami na kujigamba hii ikiwa ni baada ya kufunga pointi 33 huku 14 zikiwa katika robo ya nne. Gordon aliisaidia Utah Jazz kuibuka na ushindi wa pointi 102-91 dhidi ya Clippers.

Derrick Favors  aliongeza pointi 22, Rodney Hood 13, na Rudy Gobert alikuwa na pointi 10 na 11 rebounds huku Utah Jazz wakiweza kufikisha japo  pointi 100 kwa mara ya pili msimu huu wakati wakitoka katika mfululizo wa kupoteza michezo miwili.

Blake Griffin alikuwa na 40 pointi zikiwa ni  mbili nyuma ya pointi zake nyingi za muda wote katika mchezo mmoja pia akadaka  12 rebounds kwa CLIPPERS , ambao sasa wana rekodi ya 7-8 huku wakipoteza michezo yao saba katika mechi nane .

Clippers hawakuwahi kupigwa na Jazz tangu Januari 17, 2012 , huku ikiwa ndio rekodi yao ndefu dhidi ya wapinzani wengine.

Chris Paul aliongeza pointi 24 na kusaidia pasi  nane , na DeAndre Jordan alikuwa na 11 rebounds .

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here