Home Kitaifa Ningependa Watoto wangu waichezee Tanzania, ila sitawazuia wakiichagua Sweden’

Ningependa Watoto wangu waichezee Tanzania, ila sitawazuia wakiichagua Sweden’

649
0
SHARE

zdvfxbgchjk

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Kiungo wa zamani wa klabu za Simba SC, Mtibwa Sugar, Moro United na Azam FC, Shekhan Rashid ameweka wazi kwamba, atafurahi ikiwa motto wake wa kiume, Jamal atakuja kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars). Shekhan kwa sasa ni baba wa watoto wawili ( Jamal mwenye miaka miwili na dada yake Maryam mwenye miaka mitatu na miezi tisa)

“Nadhani Jamal anaweza kuja kuwa mchezaji mzuri wa nafasi ya kiungo. Anapenda sana mpira wa miguu, yeye pamoja na dada yake Maryam. Naona watafuta nyayo za baba yao.” Anasema mchezaji huyo wa zamani wa Taifa Stars ambaye kwa sasa anaishi nchini Sweden.

Watoto wake wote wamezaliwa katika nchi hiyo ya Scandinnavia. “Nitafurahi Jamal akija kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania ila sitamzuia ikiwa ataichagua Sweden. Mungu akituweka hai nitampeleka mwanangu katika academy za mpira ili apate mwongozo”

Mtoto wa kike wa Shekhan ( Maryam) anapenda sana mpira wa miguu na Sweden ni kati ya nchi ambazom zina timu imara za Taifa za wanawake.

“Sitamzuia mwanangu kucheza mpira wa miguu kama atahitaji. Maryam anaupenda sana mpira nitamuangalia nione atataka nini, ila akitaka kucheza mpira atacheza.” Disemba 12, Shekhan anataraji kutimiza miaka mitano katika ndoa yake na mkewe Bi. Hanaa jamal ambaye ni mama wa Maryam na Jamal.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here