Home Kimataifa Ni aina gani ya matokeo vs Porto yataivusha Chelsea kwenda 16 bora

Ni aina gani ya matokeo vs Porto yataivusha Chelsea kwenda 16 bora

713
0
SHARE

Mashabiki wa Chelsea jana waliachwa wakikuna vichwa wakifikiria ni matokeo ya namna gani yatakayoihakikishia timu yao kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya wakati watakapokutana na Porto @Stamford Bridge katika mechi ya mwisho ya kundi G.

  Baada ya matokeo ya jana usiku ambapo Porto alifungwa 0-2 Dynamo Kyiv na Maccabi Tel Aviv wakafungaa 4-0 na Cheksea – kikosi cha Jose Mourinho sasa ndio wanaongoza kundi wakiwa na pointi 10, mbele ya Porto ambao nao wana pointi 10.
Kiev, kwa upande mwingine wana 8, wakati Maccabi wakishika mkia na zero pointi.

Hivyo ni matokeo ya namna gani Chelsea watahitaji ili kujihakikishia kufuzu?
Ikiwa Chelsea na Porto watotoa sare, na Kiev akashinda vs Maccabi – timu zote zitakuwa na pointi 11 – hivyo nani ataenda raundi ya 16 bora?
Tambua wakati timu zaidi ya mbili kwenye kundi zinapokuwa na pointi zinazolingana huwa hakuna utaratibu aa kuangalia – matokeo ya head to head. Badala huwa wanaangalia tofauti ya magoli baina ya timu 3 za juu zilizofungana kipointi.

Hivyo itakuwa namna hii

1) Chelsea anahitaji sare tu kufuzu.

2) Porto itabidi ashinde tu vs Chelsea ili kujihakikishia kufuzu, sare haitoshi ikiwa Dynamo atashinda vs Maccabi.

3) Dynamo watafuzu moja kwa moja ikiwa tu wataifunga timu dhaifu ya Maccabi ambayo imepoteza mechi zake zote za kundi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here