Home Kimataifa Je Man United itafuzu 16 bora leo? Timu zinazoweza kufuzu na kutolewa...

Je Man United itafuzu 16 bora leo? Timu zinazoweza kufuzu na kutolewa leo Champions League

712
0
SHARE

Baada ya kitimutimu cha usiku wa jana wa Ligi ya mabingwa ambapo tulishuhudia FC Barcelona wakiipa kisago cha 6-1 AS Roma na kufuzu kwenda hatua ya 16 bora – leo ni zamu ya vigogo wengine kutafuta nafasi 16 na nyingine zitakuwa zikiaga mashindano au kupigania nafasi ya kwenda kucheza UEFA Cup.


Group A: Malmö (3) v Paris Saint-Germain (7), Shakhtar Donetsk (3) v Real Madrid (10, qualified)

Madrid, tayari wamefuzu na wataweza kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi ikiwa watashinda au kutoa sare na PSG wasishinde, au kama wao na PSG wote wakifungwa.

PSG watakuwa wamepita ikiwa watashinda mechi ya leo au wakitoa sare na Shakhtar wakapoteza.

Malmö inawabidi kushinda ili waweze kubakia katika mashindano ya kugombea nafasi ya mbili za juu..

Shakhtar inawalazimu kushinda na huku wakiombea PSG wafungwe ili waendelee kubaki kwenye kugombea nafasi mbili za juu.

 Group B: CSKA Moskva (4) v Wolfsburg (6), Manchester United (7) v PSV Eindhoven (6)

United watakuwa wamefuzu ikiwa watashinda vs PSV .

CSKA watakuwa hawana uwezo wa kumaliza katika nafasi mbili za juu ikiwa watafungwa.
 Group C: Astana (3) v Benfica (9), Atlético Madrid (8) v Galatasaray (4)

Benfica watakuwa wamefuzu wakishinda, au sare lakini kama Atletico wataifunga Galatasary au wakitoa sare.
Ikiwa Benfica watashinda na Atletico wasiposhinda, Benfica watakamata nafasi ya kwanza.

Atlético watafuzu endapo watapata sare tu.

Ikiwa Astana watapoteza au kutoa sare na Galatasary wakashinda,  Astana nao watakuwa wamehakikishiwa nafasi ya 4.

 Group D: Juventus (8) v Manchester City (9, qualified), Borussia Mönchengladbach (2) v Sevilla (3)

City wameshafuzu na watapata nafasi ya kwanza ikiwa watashinda mechi ya leo. Juventus watafuzu wakishinda, au endapo Sevilla watapata matokeo yoyote ambayo sio ya ushindi usiku wa leo.

Ushindi ndio njia pekee kwa Sevilla kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu wakati watakapocheza dhidi ya Juve tarehe 8 December, na endapo watashindwa kufuzu wataenda UEFA Cup – mashindano ambayo walishinda miaka miwili iliyopita.

Mönchengladbach, tayari wameshatolewa kwenye UEFA Champions League.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here