Home Kitaifa ‘Hassan Dilunga alifanya kosa kuichagua Yanga SC, anarudia tena kuiacha Stand United

‘Hassan Dilunga alifanya kosa kuichagua Yanga SC, anarudia tena kuiacha Stand United

1027
0
SHARE

Capturel

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Wakati anajiunga na Yanga SC akitokea klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani mwezi Desemba, 2013 nakumbuka nilihoji kuhusu usajili wake kiasi cha kupingwa sana na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu na kusema kuwa usajili huo ungekuwa na faida kwa kila upande. ‘ Usajili wa Mr,Kazinyingi Yanga SC, Nani atakayempisha Dilunga kikosini?’ ndiyo kilikuwa kichwa cha habari katika hoja yangu ile karibia miaka miwili sasa iliyopita.

Nilipinga na usajili ule kwa sababu, Kwanza, hayakuwa ni mapendekezo ya aliyekuwa mkufunzi wa Yanga, Ernie Brandts. Kumbuka usajili wa Dilunga ndani ya Yanga ( wakati huo 2013) uliambatana na ule wa wachezaji ‘ mastaa’ katika kandanda la Tanzania, kipa Juma Kaseja na mshambulizi, Mganda, Emmanuel okwi.

Brandts hata kabla ya kutimuliwa mwishoni mwa mwezi huo alisema kuwa usajili wa wachezaji hao watatu haukuwa mapendekezo, zaidi alisema ulikuwa ni sejemu ya kuivuruga timu yake ambayo ilikuwa na wachezaji wa kutosha.

Nafikiri, Kaseja alijiharibia baada ya kufungwa kizembe katika mechi dhidi ya Simba SC ( 3-1 Mtani Jembe, 2013) ndiyo maana alishindwa kufanya vizuri licha ya kufanya kazi na walimu, Hans Van der Pluijm na Marcio Maximo. Nafasi yake ya kwanza mbele ya Deogratius Munish ‘ Dida’ na Ally Mustapha ‘ Barthez’ ilipotelea pale, ila alikuwa na nafasi ya kucheza ndani ya Yanga hasa ukizingatia makosa makubwa ya kiuchezaji yaliyofanywa na Mustapha katika sare ya Simba 3-3 Yanga, Oktoba, 2013.

Okwi alikuwa na nafasi yake Yanga ila mambo ya kimaslai yakamuondoa mapema. Ila, Dilunga kulingana na umri wake hakupaswa kujiunga na Yanga wakati ule klabu za Azam FC na Simba pia zikimuhitaji. Yanga ilikuwa imejaa na ukitazama hadi sasa timu hiyo imejengwa kupitia Haruna Niyonzima ( mchezaji ambaye kwa lazima Dilunga alipaswa kumuweka nje). Alipata pesa, ila sasa baada ya kushindwa kucheza mara kwa mara ndani msimu mmoja na nusu ndani ya Yanga mambo yanazidi kwenda hovyo.

JKT Ruvu inaweza kuwa klabu yake ya tatu kuichezea ndani ya miwili kama tu timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa itafanikiwa kukamilisha usajili wake kutoka Stand United. Dilunga alijiunga na Stand mara baada ya kutemwa katika klabu ya Yanga mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2014/15. Ameshinda ubingwa wa ligi kuu mara moja ni heshima ya aina yake na kukumbukwa kwa mchezaji ye yote Yule.

Nafikiri kufanya kazi na mkufunzi, Abdallah ‘ King’ Kibadeni inaweza kuwa chachu ya kiungo huyo kuichagua JKT Ruvu na kuitosa timu inayofanya vizuri katika ligi msimu huu. Kitu gani kimemkimbiza Dilunga ndani ya Stand United? Kiubora wako juu zaidi ya JKT Ruvu, kimalengo wana mtazamo mpana kushinda JKT Ruvu. Je, ameshindwa kwa mara nyingine changamoto ya kuwania nafasi kikosini?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here