Home Kimataifa ZINEDINE ZIDANE AMESEMA HIVI KUHUSU YEYE KUCHUKUA NAFASI YA RAFAEL BENITEZ

ZINEDINE ZIDANE AMESEMA HIVI KUHUSU YEYE KUCHUKUA NAFASI YA RAFAEL BENITEZ

543
0
SHARE

1622E2AB000005DC-0-image-a-22_1448238461341

Baada ya mechi ya El Classico zikavuma tetesi kwamba Zinedine Zidane anatakiwa kuchukua nafasi ya Rafael Benitez kwenye club ya Real Madrid.

Tetesi hizo zilipewa kasi baada ya mchezaji wa Brazil Rivaldo ku-post kwenye instagram yake kwamba ni wakati wa Real Madrid kumpa nafasi Zidane ajaribu ku-manage club hiyo kama Pep Gurdiola alivyopewa nafasi na Barcelona.

Waandishi wa habari wamemtafuta Zidane ambae ni kocha wa kikosi cha vijana cha Real Madrid “Castilla” na yeye alijibu kama hivi, “Mimi ni kocha Castilla na Benitez ni kocha wa kikosi cha kwanza, mambo ni mazuri kwa sasa hapa Castilla. Nitaendelea kuwa kocha wa Castilla kwa muda kwasababu nafanya vitu kidogo kidogo sina haraka. Kitu cha muhimu ni kuwa na furaha kwenye kazi unayoifanya na mimi nina furaha hapa ndani ya Castilla”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here